Tuesday, August 29, 2017

Bilioni 40/- zatengwa ujenzi wa vyoo na soko la Makole D

ad300
Advertisement
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imesema itatumia Sh.milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo na maandalizi ya soko la Makole D Center.
Imesema eneo hilo ndilo lililoandaliwa ili kuwahamishia wafanyabiashara ndogo ndogo (machinga) walioko katika maeneo mbalimbali mjini hapa.

Pia imesema imeshaanza mchakato wa kuwatambua na kuwarasimisha wafanyabishara hao ili kuwapeleka kwenye maeneo yaliyotengwa maalumu kwa ajili yao.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Godwin Kunambi, alibainisha hayo mjini hapa jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema, tayari kiasi cha Sh.milioni 40 kimepitishwa na halamashauri hiyo kwa ajili ya ujenzi huo.

Tunaandaa soko Makole kwa ajili ya machinga hawa wanaofanya biashara zao barabarani na wiki iliyopita nilizungumza na mwenyekiti wao wa machinga kutoka Mwanza tunataka tuwatambue, tujue idadi yao halafu tuwarasimishe tuwapeleke pale Makole,” alisema Kunambi.

Alisema wanataka kuwahamishia wamachinga wote kwenye eneo hilo ili kupunguza kero kwenye barabara za mji.

Kunambi alisema, kuna soko jingine lipo Chadulu pia watapelekwa akina mama wanaouza mboga mboga na matunda.

Alisema lengo la kurasimisha ni kutaka tutawatambua kwa orodha ili wajue wapo wangapi, na kwamba watakaosalia watawapeleka katika soko la Bonanza lililopo katika eneo la Chamwino mjini hapa.

Mkurugenzi  huyo, alibainisha kuwa hadi kufikia Oktoba mwaka huu soko la Chadulu litakuwa tayari na mwishoni mwa mwezi septemba soko la Makole litakuwa limekamilika.

Kunambi alisema watahakikisha wanadhibiti kuzalisha wamachinga wengine makao makuu kwa kuwa watawatambua waliopo na kuwapeleka kwenye maeneo rasmi.

Tutaweka ulinzi mkubwa sana kwenye maeneo yetu ya barabara maana tusipofanya hivi itakuwa ni kero, nilifanya uchunguzi mdogo nikawa nawauliza mwingine anasema ametoka mwanza, Iringa, Singida nikisema niwaondoe hawa kwa muda watakuja wengine watakaa hivyo kero hii nitakuwa sijaizuia,”alisema

Mkurugenzi huyo alisema lengo la kuwapeleka kwenye maeneo rasmi ni kudhibiti ufanyaji biashara holela kwenye barabara za mji.

Kuhusu mapato, Kunambi alisema Halmashauri hiyo imepiga hatua kwa mwaka wa fedha uliopita kwenye makusanyo ya mapato ya ndani.

Alisema lengo lilikuwa kukusanya Sh.Bilioni 3.9 lakini zimekusanywa Sh.Bilioni 4.6 kwa hiyo ukusanyaji umefikia wa asilimia 117.

Kwa hiyo kwa mwaka wa fedha uliopita 2016/17 utaona tumevuka lengo kwa asilimia 17, lakini pia fedha tulizopeleka kweye miradi ya maendeleo kupitia mapato ya ndani ni Sh.Bilioni 1.2,”alisema Kunambi.

Alisema Manispaa hiyo imeweza kutumia mapato yake ya ndani kujenga miundombinu tofauti na Halmashauri zingine nchini.

Imeandikwa na Happiness Mtweve aliyeko Dodoma.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: