Tuesday, August 29, 2017

Ni mtifuano mawakili wa NASA, IEBC na Jubilee mpaka kieleweke

ad300
Advertisement
Mvutano umeibuka katika Mahakama ya Juu ya Kenya kati ya mawakili wa NASA, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na wale wa Rais Uhuru Kenyatta kuhusu utekelezaji wa agizo la kukagua mitambo ya tume lililotolewa juzi Agosti 28 na mahakama hiyo.

NASA kupitia kwa wakili wake ilidai kwamba IEBC haikuwa ikitelekeza agizo hilo kikamilifu hasa kwenye suala lililohusisha ukaguzi wa mitambo ya kuhifadhi taarifa za tume hiyo.
 

Tunataka IEBC kutii agizo la mahakama kikamilifu. Kufikia sasa hawajafanya hivyo na muda unakwisha,” alisema Wakili James Orengo anayemwakilisha Raila Odinga.

Kauli yake inafuatia agizo la majaji wa Mahakama ya Juu kwa IEBC, lililotaka tume hiyo kuruhusu wataalamu wa NASA kukagua mitambo yao chini ya usimamizi wa wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) walioteuliwa na Mahakama.

Hata hivyo, NASA ilisema maofisa wa IEBC hawakutekeleza kikamilifu agizo hilo wakisema walipiga kambi katika ofisi za IEBC hadi saa kumi na nusu Jumatatu usiku.

Lakini upande wa IEBC, wakili wake Paul Muite, alisema NASA ilitoa matakwa ambayo hayakuwa kwenye agizo la mahakama.

Alisema mitambo ya IEBC iko Ulaya na walihitaji muda ili kulitekeleza tofauti na inavyotaka NASA.

Ninahakikishia mahakama kwamba tutatekeleza agizo la mahakama kikamilifu,” alisema wakili huyo.

Muite aliiomba mahakama kuagiza msajili wa mahakama ya juu kuongeza idadi ya wafanyakazi wanaokagua fomu 34A na 34B akisema shughuli hiyo ilikuwa ikiendelea pole pole sana.

Naye Wakili Fred Ngatia, anayemwakilisha Rais Mteule Uhuru Kenyatta, alisema shughuli hiyo ilikuwa ikiendelea vyema na kuilaumu NASA kwa kutoa matakwa ambayo hayakuwa kwenye agizo la mahakama.

Kwa upande wa mahakama, Jaji Mkuu David Maraga alikubali ombi la NASA kuiagiza IEBC kufanya ukaguzi huo haraka na aliionya IEBC kwamba inapasa kutekeleza kikamilifu agizo la mahakama hiyo.
 

Tunachotaka ni utekelezaji kikamilifu wa agizo hilo. Wakili Muite, mwambie mteja wako kwamba tunataka agizo litekelezwe na lisipotekelezwa tutaamua hatua tutakazochukua,” alisema Jaji Mkuu.

Maamuzi ya mwisho ya kesi hiyo inayopinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 8, mwaka huu iliyofunguliwa na muungano wa NASA, yanatarajiwa kutolewa Ijumaa wiki hii.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: