Advertisement |
Kiongozi wa muungano wa NASA aliyegombania urais wa Kenya kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo Agosti 8, mwaka huu, Raila Odinga amewasilisha kesi mahakama kuu ya Kenya.
Shauri hilo ni la kuiomba mahakama hiyo ya juu kubatilisha ushindi wa Rais mteule Uhuru Kenyatta aliyetangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) katika uchaguzi huo kwa zaidi ya kura milioni 8.
Odinga amesema mchakato mzima wa kurekodi, kusafirisha, kuhakiki na kuthibitisha kura ulikuwa na makosa mengi, hivyo matokeo sahihi hayakupatikana.
Awali alinukuliwa akisema yeye ndiye mshindi sahihi wa uchaguzi huo na si kama ilivyoamuliwa na IEBC.
Mbali na madai hayo, Odinga anakabiliwa na wakati mgumu kutokana na taarifa za waangalizi wote wa kimataifa wa uchahuzi kukiri kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki.

0 comments: