Sunday, August 20, 2017

Watuhumiwa wa ugaidi Barcelona mbaroni

ad300
Advertisement
Watu wawili wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na shambulizi la kigaidi nchini Hispania.

Tukio hilo lililoteka juzi baada ya gari moja kuvamia watu waliokuwa wakitembea kwa miguu katika eneo maarufu la kitalii la Las Ramblas jijini Barcelona.

Kutokana na tukio hilo, watu 13 wamethibitishwa kufariki na wengine zaidi ya mia moja wamejeruhiwa, wengi wao wakiwa katika hali mbaya.

Idara ya polisi ya jiji hilo, imesema dereva wa gari hilo si mmoja wa watu hao wawili waliokamatwa, na mpaka sasa hajulikani aliko. 

Waziri mkuu wa Hispania Mariano Rajoy, amelaani shambulizi hilo na kutangaza siku tatu za maombolezo. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres pia amelaani vikali shambulizi hilo.

Kundi la kigaidi la IS limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: