Thursday, August 31, 2017

Edouard Nigirente ala kiapo kuwa Waziri Mkuu Rwanda

ad300
Advertisement


Takriban mwezi mmoja baada ya uchaguzi mkuu wa Rwanda uliompa ushindi Rais Paul Kagame, amemteua na kumwapisha Waziri mkuu wake mpya Edouard Nigirente.

Hafla ya kuapishwa kwa waziri mkuu huyo, imefanyika leo Agosti 31, jijini Kigali, makao makuu ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.


Katika hafla hiyo, Rais Kagame alisema ana imani na uwezo wa Nigirente na nia yake ya kufi kia mafanikio wanayoyatarajia wananchi wa Rwanda.


Naye Nigirente (pichani), alisema yuko tayari kujituma kwa uwezo wake wote kwenye kutekeleza majukumu aliyopangiwa kikatiba kwa manufaa ya wananchi wa Rwanda waliochagua serikali yao Agosti 4, mwaka huu.
 

Kwa mujibu wa katiba ya Rwanda, waziri mkuu anateuliwa ndani ya siku 15 baada ya rais mpya kuapishwa, huku mawaziri wengine wakitakiwa kuteuliwa ndani ya siku 15 tangu kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: