Sunday, August 20, 2017

Atumia Mil 11.4/- kununua chakula mgahawani

ad300
Advertisement
Mtu mmoja nchini China amewashangaza watu kwa kutoa Sh. Milioni 11.4, kununulia watu sahani za chakula kutokana na furaha ya kuipata pete aliyoipoteza yenye thamani ya Sh. Milioni 96 (Dola 44,000 za Marekani).

Alitumia fedha hizo kulipia sahani 5,000 za chakula kwenye mgahawa ulio kusini magharibi mwa nchi hiyo katika mji wa Chongqing, baada ya kuipata pete hiyo ya almasi aliyokuwa ameinunua maalumu kwa mpenzi wake.

Kwa mujibu wa gazeti Chongqing Morning Post, mwanamume huyo Wang, alikuwa na nia ya kum 'suprise' mpenzi wake kwa pete hiyo ya uchumba, baada ya kuwa naye kwa mwaka mmoja na kabla ya kufanya hivyo ilipotea.

"Nilifanya maandalizi ya mpango huo lakini wakati nilipokuwa nakula chakula cha mchana, niliondoka kwenye kiti dakika chache kwenda kupokea simu na niliporudi pochi yangu ilikuwa imeibwa," alisema.

Alisema huku akiwa amechanganyikiwa asijue cha kufanya, aliondoka mgahawani hapo na kurudi nyumbani ambako baada ya saa chache alijulishwa kwa simu kuwa mkoba wake umepatikana.

"Nilifahamishwa kuwa uliokotwa na mfanyakazi mmoja wa mgahawa ule na akaukabidhi kwa meneja wake Yue Xiaohua ambaye ndiye alinipigia simu.

"Niliufuata mkoba wangu siku ile ile na kukuta baadhi ya vitu vimeibwa lakini pete ipo, ndipo kwa furaha nikaulizia idadi ya sahani za chakula wanazouza kwa siku," alisimulia.

Baada ya kujulishwa na Meneja kuwa kama siku ni nzuri kibiashara huwa wanauza takriban sahani 5,000 zinazogharimu jumla ya dola 5,200 (Sh. Milioni 11.4)aliagiza kila mtu aalikwe kula chakula kisha akalipa gharama hizo.

Gazeti hilo pia lilisema kuwa Wang aliandika barua ya kushukuru mgahawa huo akisema kuwa mpenzi wake aliikubali pete hiyo na kuahidi kufunga naye ndoa.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: