Advertisement |
Ikiwa ni miezi michache tangu Zanzibar kukubaliwa ombi lake la kuwa mwanachama wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), imepokonywa uanachama huo.
"Walipokelewa bila ya kufuatwa kwa sheria za shirikisho ambazo ziko wazi," amesema Ahmad.
Aliongeza kuwa CAF haiwezi kukubalia uanachama wa mashirikisho mawili kutoka kwa taifa moja.
"Ufafanuzi wa maana ya taifa unatoka kwa Muungano wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa," alisema Ahmad katika mkutano mkuu maalumu wa shirikisho hilo nchini Morocco.
FIFA kwa upande wake ilikataa kuipokea Zanzibar kama mwanachama hata baada ya hatua ya CAF, iliyoidhinishwa na mtangulizi wa Ahmad kwenye nafasi ya uenyekiti, Issa Hayatou.
Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini imekuwa ikiendesha shughuli zake za soka kivyake na kuwakilishwa katika mashindano ya soka ya kanda.
0 comments: