Advertisement |
Shirika la Umoja wa Mataifa
la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), limezindua Mpango Mkakati wa Nchi (CSP) wa
Tanzania utakaodumu kwa miaka minne na kusaidia zaidi ya watu 900,000.
Mpango huo unaendana na Ajenda
ya Umoja wa Mataifa wa 2030 ya Maendeleo Endelevu, inayolenga kuondoa umaskini, kupunguza
tofauti ya usawa, kukabili mabadiliko ya tabia ya nchi na kuhakikisha kunakuwa
na kilimo endelevu na usalama wa chakula.
Hayo yalisemwa jana Dar es Salama na Michael Dunford, Mwakilishi wa Nchi wa WFP
Tanzania, ambaye aliongeza kuwa WFP inakusudia kuimarisha uwezo wa kupata soko kwa wakulima
wadogowadogo 250,000.
"Utekelezaji wa mpango huu umeanza Julai 1, mwaka huu baada ya kupitishwa na
Bodi Tendaji ya WFP," alisema.
Pia a
lisema pia programu ya lishe inayohusisha sekta
mbalimbali kwa akina mama 185,000 na kutoa msaada wa chakula kwa zaidi ya wakimbizi
300,000 itaendelea ili kuwapa mazingira salama wenye uhitaji hususan wa chakula.
Aliongeza: "
Umesanifiwa ili kuwezesha uwekaji mipango wa muda mrefu ili kuunga mkono Mpango
waPili wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II) na Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa Serikali wa Miaka Mitano."
Akizungumzia mpango huo, Brigedia Jenerali Mbaazi Msuya ambaye ni Mkurugenzi wa Idara
ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, alisema utayarishaji wake unaipa Serikali fursa ya kuchagua maeneo ya
kipaumbele.
"Tunapata fursa ya kupanga kipi kianze ambako kwa kushirikiana na washirika wetu, itaweza kupunguza matokeo ya
majanga kwa watu walio hatarini ili waweze kujinusuru na kujiletea usalama
zaidi wa chakula," alisema.
Mkazo katika kazi za WFP
, umetajwa kulenga dharura na msaada wa chakula
ambapo asilimia 85 ya bajeti
ya Shirika ya miaka minne ya Dola za Marekani milioni 455.7 imetengwa kusaidia
wakimbizi wapatao 310,000 pamoja na jamii za wenyeji kaskazini-magharibi mwa
Tanzania.
0 comments: