Wednesday, July 26, 2017

10 wapelekwa China kusoma ICT

ad300
Advertisement
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dk. Leonard Akwilapo, amesaini makubaliano na Jamhuri ya Watu wa China - (MOU) ya kuwasafarisha wanafunzi Kumi kutoka Tanzania kwenda nchini China kujifunza Taaluma ya Mawasiliano na Teknolojia, ICT - kupitia Makao makuu ya Kampuni ya simu ya Huawei ya nchini humo kwa wiki tatu.
 

Akizungumza na wanafunzi wanaotarajiwa kuhudhuria mafunzo hayo mjini Dodoma, Dk. Akwilapo amewataka kuhakikisha wanakwenda kujifunza na kuangalia Maendeleo ya kompyuta ili waje kuendeleza ufundi na ujuzi wa Teknolojia watakayokuwa wameipata nchini China.
 

Hii ni mara ya Pili kwa Makao Makuu ya Huawei ya nchini China kusafirisha wanafunzi kwenda nchini humo kwa ajili ya mafunzo hayo ya kompyuta lengo likiwa ni kuwajengea vijana uwezo katika sekta ya mawasiliano.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: