Advertisement |
Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo umetangaza mipango na mikakati yake mipya ya kushinikiza kuondoka
madarakani kwa Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo kwa kutumia migomo na uasi
wa kiraia.
Taarifa ya kambi ya upinzani nchini humo imeeleza kuwa wapinzani wanaendelea
kufanya maandamano na kuhamasisha uasi wa kiraia ili kumshinikiza Rais
Kabila aachie ngazi na kuondoka madarakani.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Agosti 20 mwaka huu, upinzani umepanga kufanya maandamano mfululizo katika mji mkuu Kinshasa na majimbo 25.
Tangazo hilo linakuja baada ya siku
mbili za mazungumzo ya upinzani jijini Kinshasa, kufuatia wasiwasi kuwa
Rais Kabila anayetawala taifa hilo tangu mwaka 2001 huenda akaendelea
kubakia madarakani na hivyo kukiuka hata makubaliano yaliyofikiwa mwaja
jana.
Uchaguzi ulitakiwa kufanyika mwaka huu
katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa mujibu wa mkataba
uliokusudia kuepusha vurugu za kisiasa nchini humo baada ya Rais Kabila
kuendelea kubakia madarakani hata baada ya muhula wake wa uongozi
kumalizika Disemba mwaka jana.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Agosti 20 mwaka huu, upinzani umepanga kufanya maandamano mfululizo katika mji mkuu Kinshasa na majimbo 25.
Mgogoro wa ndani nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo uliibuka baada ya kuahirishwa tarehe ya uchaguzi
wa rais na kadhalika sisitiza la Rais Joseph Kabila la kutaka kuendelea
kusalia madarakani nchini humo.
Licha ya kutiwa saini makubaliano baina
ya wapinzani na serikali juu ya kufanyika uchaguzi wa rais tarehe 31
mwezi Disemba mwaka huu, hata hivyo inaonekana kuwa, uchaguzi huo
hautaweza kufanyika katika tarehe iliyopangwa.
0 comments: