Advertisement |
Jengo la bunge la Ujerumani |
Chama cha CDU kimekuwa kikipinga ndoa za aina hiyo huku pia kiongozi wake, Angela Merkel akinukuliwa kutangaza waziwazi kipindi cha nyuma kuwa anapinga suala hilo ingawa aliwaruhusu wabunge wa chama hicho kupiga kura bungeni kwa mujibu wa mitazamo yao binafsi.
Katika hatua hiyo, wabunge 225 kati ya 309 wa chama cha Christian Democratic Union walipiga kura ya hapana dhidi ya muswada wa sheria hiyo.
Sheria inayoruhusu ndoa ya watu wenye jinsia moja nchini Ujerumani ilitiwa saini juzi na Rais Frank-Walter Steinmeier wa nchi hiyo na itaanza kutekelezwa rasmi Oktoba Mosi mwaka huu.
Ikumbukwe kuwa mwezi uliopita, Bunge la Ujerumani, Bundestag liliipitisha sheria inayoruhusu ndoa za watu wa jinsia moja na kutambua rasmi haki ya watu wanaojihusisha na ngono ya jinsia moja kulea watoto nchini humo.
Kwa utaratibu huo, Ujerumani sasa inakuwa nchi ya 21 ya bara Ulaya kupitisha sheria ya ndoa baina ya watu wenye jinsia moja Denmark ikiweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kupitisha sheria kama hiyo mwaka 1992.
0 comments: