Advertisement |
Timu ya soka ya Azam ya jijini Dar es Salaam imeshindwa kuonyesha ufundi wake wa kusakata kabumbu baada ya kufungwa goli 2-0 na Njombe mji.
Mchezo huo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, umechezwa kwenye uwanja wa Makambako, mkoani Njombe.
Akizungumza kwa simu kutoka Njombe, Msemaji wa Azam Jaffar Idd, amesema wamekubali kichapo hicho na kuipongeza Njombe Mji kwa ushindi.
"Ulikuwa mchezo mzuri, vijana wamecheza vizuri lakini ndo hivyo mpira wa miguu una matokeo matatu na haya ya leo ni matokeo," alisema.
Msemaji huyo alisema baada ya mchezo huo na Njombe Mji, Julai 26 watacheza na Lipuli ambayo pia imepanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao kabla ya kurudi Dar es Salaam.
0 comments: