Advertisement |
Rais Vladmir Putin wa Russia na Donald Trump wa Marekani |
Sheria hiyo pia itapunguza uwezo wa Rais Donald Trump wa kuiondolea nchi hiyo vikwazo.
Kipindi cha Trump ofisini kimekumbwa na madai kuwa Russia ilisaidia kushawishi uchaguzi wa mwaka uliopita wa nchini Marekani.
Hata hivyo Russia inakana kutenda jambo lolote baya la uchunguzi ambao umefanywa na Marekani ambao una lengo la kutathmini ikiwa kuna yeyote katika kampeni ya Trump alishirikiana na maafisa wa Russia kudukua uchaguzi huo.
Waandishi wa habari wa Marekani walisema kuwa makubaliano hayo ya Congress, yanaonyesha msimamo uliopo dhidi ya Russia bila kujali maoni ya Rais Trump.
Inasemekana kuwa Rais Trump anaweza kuukataa mswada huo, lakini kwa kufanya hivyo anaweza kushukiwa kuwa anaiunga mkono Russia.
Aidha, kwa upande mwingine inaelezwa kuwa endapo atautia sahihi mswada huo itakuwa ni kuidhinisha sheria ambayo utawala wake unaipinga.
Mswada huo pia unaruhusu vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini na Iran.
Kwa ujumla, sheria hiyo inadaiwa kuwa itaruhusu vikwazo vipya dhidi ya Urusi kwa kulimega eneo la Crimea mwaka 2014 na madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani.
0 comments: