Advertisement |
Ni game ya kirafiki itakayopigwa kama moja maandalizi na kipimo kwa timu zote mbili kuelekea kwenye pilika pilika za ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.
Joto la mechi hii limeanza kupanda kwa baadhi ya mashabiki, wapenzi wa soka hapa nchini kutokana na hali ilivyo kwenye suala zima la usajili kwenye timu zote mbili.
Yanga wanataka kutunza heshima yao ya kuwa mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu ambalo imelitwaa mara tatu mfululizo tangu msimu wa 2014/2015.
Kwa upande wao Singida United, ikiwa ni timu changa kabisa kwenye orodha ya timu 16 za livi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, itashuka dimbani kutaka kuifundisha adabu Yanga ili kutuma salamu kwa timu zingine zinazodhani timu hiyo itakuwa ya kujikusanyia pointi.
Ngoja tusubiri, tuombe uzima na afya ili kuja kuuona uhondo huu unaotarajiwa kutokana na ufundi na uzoefu wa walimu wa timu zote mbili.
0 comments: