Advertisement |
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa amesema safari ya Watanzania kuachana na nguo za mitumba imewadia kutokana
na uwepo wa viwanda vya kutengeneza nguo nchini.
Pia amesema uwepo wa
viwanda hivyo utasaidia wakulima wa pamba kupata soko la uhakika hivyo
amewataka walime pamba ya kutosha ili viwanda husika vipate malighafi za kutosheleza uzalishaji kwa mwaka mzima.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Julai 15, 2017) wakati
alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Namera kilichoko Gongo la Mboto na kiwanda
cha nguo cha Nida kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam.
Alisema viwanda vya kutengeneza nguo nchini ni
ushahidi tosha kwamba nchi iko njiani kuondokana na matumizi ya nguo za mitumba
kwa kuwa nguo nyingi zitakuwa zinatengenezwa nchini, hivyo kupatikana kwa bei
nafuu.
Alisema kwa sasa wanunuzi wa pamba hawana sababu ya
kwenda kuuza nje ya nchi na badala yake wauze katika viwanda vya ndani ili
vizalishe nguo za kutosha zitakazouzwa nchini kwa gharama nafuu.
“Pamba yote inaweza kuchakatwa nchini, hivyo hakuna
haja ya kuiuza nje ya nchi. Natoa wito kwa wakulima wetu wa pamba walime mazao
ya kutosha kwa sababu soko la uhakika ipo na hii ndio safari ya mwisho ya mitumba.”
Awali
Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha saruji cha Lake kinachozalisha saruji
ya nyati ambapo aliwapongeza wawekezaji wote nchini kwa kuunga mkono jitihada
za Rais Dkt. John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda.
Katika kiwanda hicho ambacho kinazalisha tani
700,000 kwa mwaka kimeajiri watu 2000 na kinalipa kodi ya sh. bilioni 81.312 kwa mwaka, Waziri Mkuu
aliwataka watumishi wake wawe waaminifu, wafanye kazi kwa weledi na wawe
waadilifu.
0 comments: