Advertisement |
Tanzania imetajwa kuwa nchi ya 3 kwa kuwa na Taasisi za utafiti zinazofanya tafiti nyingi za kughushi (Fake Research) duniani.
Katika orodha hiyo Tanzania imetanguliwa na Nigeria na Malaysia zilizoshika nafasi mbili za juu.
Ripoti iliyotolewa na mtandao wa "TheRich" wenye makao yake mjini Oklahoma, nchini Marekani, imetaja nchi 10 mashuhuri duniani kwa kufanya tafiti "fake" na kutoa matokeo ya kutunga (Research Fraud - Inauthentic and Fake reports - Leading Countries).
Ripoti hiyo ya uchunguzi inaonesha kuwa nchi hizo ni mashuhuri kwa kufanya tafiti za uongo na kupika matokeo.
Inaelezwa kuwa mara nyingi baadhi ya mashirika hutumia kivuli cha utafiti ili kupenyeza "agenda zao binafsi au za wafadhili wao" katika ripoti za tafiti hizo.
Imeelezwa kuwa "watafiti" hujifungia vyumbani na kubuni utafiti kisha kuandika ripoti ya kubuni (fake) na kuitangaza hadharani kuwa ni matokeo halisi ya utafiti.
Orodha kamili ya nchi 10 mashuhuri kwa ubadhirifu/wizi/udanyanyifu/upikaji wa matokeo ya tafiti/utoaji wa ripoti "fake" za utafiti ni kama ifuatavyo:
1. Nigeria
2. Malaysia
3. Tanzania
4. Gambia
5. Madagascar
6. Malawi
7. Uganda
8. Benin
9. Bangladesh
10. Haiti
Nchi zote katika orodha hiyo zipo pia kwenye orodha ya nchi 25 maskini zaidi duniani iliyotolewa na UNDP isipokua Malaysia na Nigeria.
Nchi 7 katika orodha hiyo zipo Afrika, na 2 zinatoka Afrika Mashariki.
0 comments: