Thursday, June 1, 2017

Tanzania, Kenya kushirikiana kudhibiti tumbaku

ad300
Advertisement
Wizara ya afya ya Kenya imetangaza mwongozo wa kupunguza matumizi ya tumbaku na kuimarisha matibabu ya magonjwa yanayotokana na matumizi ya tumbaku. 

Katibu mkuu wa wizara ya afya ya Kenya, Julius Korir, amesema idadi ya vifo vinavyosababishwa na matumizi ya tumbaku imeongezeka na inahitaji kuanzisha njia ya kudhibiti tumbaku kama vile kutoa huduma za kuwasaidia watu kuacha kutumia tumbaku. 

Takwimu zinaonyesha kuwa watu milioni 2.5 wa Kenya wanatumia tumbaku, ambayo ni asilimia 13.3 wa idadi ya jumla ya nchi hiyo.

Serikali ya Tanzania pia imesema itatekeleza sheria mpya ya kudhibiti magonjwa yanayosababishwa na matumizi ya tumbaku. 

Waziri wa afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu, alisema sheria hiyo inalenga kudhibiti magonjwa yanayosababishwa na tumbaku kama vile saratani, ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa moyo na ugonjwa wa mapafu.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: