Monday, September 12, 2016

Wabunge vijana wataka sera ya elimu itoe jibu ukosefu wa ajira

ad300
Advertisement
Mbunge wa Jimbo la Mlalo (CCM), Rashid Shangazi
Umoja wa Wabunge Vijana wa Bunge la Tanzania (TYPG), umeiomba serikali kuangalia upya na kuboresha sera ya elimu nchini ili iwawezeshe wahitimu kujiajiri.

Wakizungumza mjini Dodoma katika kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Morena, baadhi ya wabunge hao walilalamikia mfumo na sera ya elimu na kusema unawanyima wahitimu fursa ya kujiajiri wanapomaliza masomo.

Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi, alizungumzia makuzi ya vijana kwa sasa, kwa kusema wengi wamepoteza uadilifu na kukimbilia mjini bila kuaga wala wanachokifuata hawakijui, ambapo aliwashauri wazazi kuwasimamia, kuwaonya na kulinda mila na desturi.

Kwa Upande wake, mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba, alisema imefi ka hatua vijana kwa umoja wao bila kujali itikadi za kisiasa, wawe wamoja na kulisemea kwa uchungu bungeni lao suala la changamoto ya ajira.

Alishauri vijana kujitambua kuwa wao ni Watanzania na kuhakikisha vyama haviwagawi wala haviwawekei mipaka.

Naye Agness Malo, aliwasihi vijana kuwa wamoja na kuimarisha mshikamano ili hatimaye waweze kufi ka mahali pazuri, hususan kupigania utatuzi wa changamoto zao, likiwemo suala la uhaba wa ajira.

Alisema katika uchaguzi vijana, wamekuwa wakipata changamoto kubwa, kwani wanapokuwa hawana pesa ni vigumu kushinda na hivyo kuwafanya vijana wengi kuwa waoga kuiongia kwenye siasa.

Katibu wa Umoja huo, Stephen Masele, alisema haoni chama chochote cha siasa kama kinastahili kuingia katika masuala yenye manufaa ya vijana na kukwamisha utekelezaji wake.

Masele ambaye pia ni mbunge wa Shinyanga Mjini, alisema wabunge vijana wana wajibu wa kushawishi ndani ya vikao vyao vya wabunge ndani ya vyama, kueleza, kuishauri na kuibana serikali iweze kufanya vitu ambavyo wanaona vinafaida kwa vijana wanaowawakilisha.

Alishauri kuboreshwa kwa sera ya elimu nchini, ili kumwandaa mwanafunzi tangu awali ajue anakwenda kuwa nani baada ya kuhitimu jambo alilosema lilikuwa likifanyika huko nyuma.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: