Thursday, September 15, 2016

Mbunge Aysharose aibana serikali kuhusu dawa

ad300
Advertisement
Mbunge Aysharose Mattembe (Viti Maalumu-CCM), ameibana serikali bungeni akitaka kuelezwa ni lini itaielekeza Bohari ya Dawa (MSD), kufungua duka la dawa kwenye Hospitali ya Rufani ya mkoa wa Singida.
Pia, ameitaka serikali kueleza ni lini itasambaza vifaa tiba na dawa za kutosha kwenye hospitali hiyo na zile za wilaya kutokana na kuhudumia wagonjwa wengi kila kukicha.
Katika swali lake la msingi, Aysharose alisema hospitali hizo hazina vifaa tiba na dawa za kutosha hivyo, wananchi kushindwa kupatiwa huduma bora ikiwemo wajawazito.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk. Hamis Kigwangalah, aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kutenga fedha kwenye mgawo unaotolewa na serikali kwa ajili ya kununua baadhi ya vifaa.
Alisema serikali ina utaratibu wa kuzipatia hospitali ikiwemo ya mkoa wa Singida fedha kila robo mwaka hivyo, ikiongeza na zingine kutoka kwenye vyanzo vyake ikiwemo Mfuko wa Bima ya Afya, itakuwa na uwezo wa kujitegemea kwenye baadhi ya mambo.
Alisema kwa uyaratibu huo, uongozi wa hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa kununua vifaa tiba na vitendea kazi ikiwemo vitanda vya kujifungulia wajawazito.
Kuhusu uanzishwaji wa duka la dawa la MSD, ambalo litakuwa likiuza dawa kwa bei nafuu tofauti na yale ya binafsi, Dk. Kigwangalah alisema MSD ilikubaliana na TAMISEMI kuwa hospitali zilizo chini yake zifungue maduka wenyewe na MSD itakuwa ikitoa ushauri wa kitaalamu pamoja na kuyauzia madawa na vifaa tiba kwa bei ya serikali.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: