Saturday, September 17, 2016

Radio 5 'OUT' miezi mitatu, Magic yapewa onyo

ad300
Advertisement
Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imekifungia rasmi kituo cha Radio 5, Arusha na kukipiga faini ya sh. milioni tano kw

Pia kamati hiyo imetoa onyo kali kwa kituo cha Radio cha Magic FM cha Dar es Salaam na kukitaka kiombe radhi kwa Rais Dk. John Magufuli, kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia leo.

Maaamuzi hayo yametolewa ikiwa ni wiki chache tangu Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Nape Nnauye, kutangaza kuvifungia vituo hivyo kwa muda usiojulikana hadi kamati ya maudhui itakapokamilisha uchunguzi wake.

Katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, Nape alisema uamuzi huo umefikiwa kutokana na kukiuka kanuni (maudhui) ya utangazaji ya mwaka 2005.

Akitoa uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam,  Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Joseph Mapunda alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kukaa na pande zote mbili na kutoa utetezi wao.

Mapunda alisema kwa upande wa Kituo cha Utangazaji Radio five, kinatuhumiwa kuruhusu maneno ya kashfa zilizolenga kumdhalilisha Rais  Dk. John Magufuli kupitia kipindi hake cha Matukio kinachorushwa hewani Agosti 25, mwaka huu kati ya saa 2.00 na 3.00 usiku.

Alisema katika kosa la kwanza kupitia kipindi hicho Mbunge wa Arusha Godbless Lema alitamka maneno ya kashfa kwa Rais na kituo hicho kuyarusha hewani.

Katika kosa la pili kituo hicho kinadaiwa kuyarusha hewani maneno ya uchochezi yaliyokuwa yakitolewa na Lema kuhamasisha wananchi kushiriki maandamano ‘ukuta’Septemba Mosi, mwaka huu.

Aidha alisema wakati wakirusha kipindi hicho hewani tayari jeshi la polisi lilishapiga marufuku hivyo Lema alikuwa akitoa maneno hayo ili wananchi wapambane na jeshi la polisi na kusababisha uvunjifu wa amani.

“Septemba 9, mwaka huu uongozi wa Radio 5,uliitwa mbele ya kamati hii kwaajili ya kutoa utetezi wao kwa nini wasichuliwe hatua za kisheria  na tuhuma za kukiuka kanuni za huduma za utangazaji  (maudhui) za mwaka 2005.

Katika utetezi wao uongozi huo ulikiri kuwa maudhui yaliyotangazwa kwenye kipindi yalikuwa kinyume na taratibu za sheria za utangazaji ,”alisema.
Pia alisema walidai kilichowaponza ni watangazaji wao kuwa na fikra kwamba anayetamka maneno ndie atakae wajibishwa.

Aidha alisema kipindi chao hakikuwa na nia ya kufanya makosa hayo hivyo wanaomba radhi kwa mwonekano wowote wa makosa katika kipindi kilichorushwa Agosti 25, mwaka huu.

Alisema kamati hiyo baada ya kusikiliza na kutafakari kwa kina maelezo ya utetezi huo huo na kwakuzingatia hatua zilizochukuliwa mara baada ya kupata maelekezo kutoka TCRA, imeridhika kuwa kipindi cha matukio hakikuzingatia kanuni za huduma za utangazaji.

Kutokana na makosa hayo Radio 5, imefungiwa kwa miezi mitatu kuanzia jana, imetozwa faini ya sh. milioni tano ambayo inatakiwa kulipwa ndani ya siku 30.

Pia  itakuwa chini ya uangalizi maalumu kwa muda wa mwaka mmoja  baada ya kumaliza muda waliofungiwa.

Kwa upande wa Radio Magic  imetuhumiwa kupitia kipindi chake cha Morning Magic kwenye kipengele cha kupaka Rangi kilichorushwa hewani Agosti 17, mwaka huu kati ya  saa 1.00 na saa 2.00 asubuhi.

Mapunda alisema kuwa watangazaji wa kipindi hicho walitoa maudhui yenye kukebehi yaliyolenga kumdhalilisha Rais, taasisi ya urais na serikali kwa ujumla.

Alisema maudhui hayo yalikuwa yanalenga kupandikiza fikra za chuki zenye mwelekeo wa kusababisha uvunjifu wa amani na kuhatarisha usalama wa Taifa.

Pia alisema watangazaji hao walitamka maneno ya kupinga, kudhihaki na kukejeli jitihada, amri halali zinazotolewa na vyombo vya dola.

Pamoja na hayo alisema kipindi hicho kilitoa fursa kwa wasilizaji kuchangia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maeneo kupitia simu ya mkononi.

“Moja ya ujumbe uliosomwa na mtangazaji wa kipindi hicho yalikuwa ya dharau,chuki, kebehi na uchochezi jambo ambalo lililenga kuingiza nchi katika machafuko na kuhatarisha amani na usalama wa Taifa.

Hata hivyo mwandishi aliendelea kutoa maneno ya uchochezi jambo ambalo lilikiuka kanuni za utangazaji za mwaka 2005,”alisema.

Mapunda alisema Septemba 9, mwaka huu uongozi wa Radio Magic uliitwa mbele ya kamati hiyo ili kutoa utetezi wao kabla ya hatua kali za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.

Alisema uongozi huo ulidai baada ya kusikilizishwa kipindi hicho walibaini kuna mapungufu katika kipindi cha Morning Magic kutoka kwa watangazaji na wachangiaji.

Baada ya kubaini mapungufu hayo alisema uongozi huo ulichukua hatua ya kuomba radhi na kubainisha kuwa kimsingi hayakukusudiwa wala sio msimamo wa kituo hicho.

Mwenyekiti huyo alisema walidai kuwa kituo chao sio cha kisiasa na kwamba jambo lililotokea halikukusudiwa na ikiwezekana hakitajihusisha na masuala ya siasa tena.

Pia alisema walidai baada ya kufanya tathimini kipindi cha Morning Magic kipengele cha kupaka rangi ndio kina matatizo hivyo walikusudia kukiondoa.

Aidha alisema katika majumuisho ya utetezi wao Meneja wa vipindi wa Radio Magic, Hamid Abdulrahman alidai kwa mara nyingine tena anaomba radhi na hatarajii kukosea tena na hatua za kinidhamu zimeshachukuliwa dhidi ya watangazaji wawili waliokuwa wamehusika.

Mapunda alisema baada ya kamati kusikiliza utetezi huo walibaini mambo mengi yaliyofanyika kwenye kipindi hicho.

“Maamuzi yaliyofikiwa dhidi ya Radio Magic ni kumwomba Rais, wasilizaji na wananchi wote kwa ujumla  msamaha kwa siku tatu mfululizo na tangazo hilo litolewe kwenye habari ya saa 10.00 alasiri na saa 3.00 usiku.

Tangazo hilo linatakiwa kuanza leo hadi Septemba 19 mwaka huu na wanatakiwa kulipa kipaumbele kikubwa katika taarifa za habari za muda huo,”alisema kaimu mwenyekiti huyo.

Aidha kwa Radio zote mbili zilitakiwa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo ndani ya siku 30, kama watakuwa hawajaridhia.

a kukiuka kanuni za huduma za utangazaji (maudhui) ya mwaka 2005.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: