Saturday, September 17, 2016

24,616 wakosa nafasi elimu ya juu 2016/17

ad300
Advertisement
Wahitimu 24,616 wa kidato cha sita ambao wametuma maombi Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), kupitia mfumo maalumu wa kietroniki (CAS) wamekosa nafasi ya vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Kati ya wanafunzi hao, 16,472 sawa na asilimia 35 walikuwa na sifa za kujiunga na vyuo vikuu huku 8,144 hawakuwa na sifa za kujiunga kupitia TCU.

Akizungumza jijini Dar es Saalam, Kaimu Mkurugenzi wa TCU, Profesa Eleuther Mwageni alisema matokeo ya awali yameonesha kuwa jumla ya waombaji wote ilikuwa 55,347 ambapo waombaji wenye sifa ni 47,203 sawa na asilimia 85.3
Profesa Mwageni alisema katika waombaji hao wenye sifa waliopata vyuo ni 30,731 sawa na asilimia 65 ambapo waombaji wenye sifa 16,472 hawajapata vyuo hadi sasa.

Alisema uchambuzi unaonesha kuwa waombaji wengi wamependelea baadhi ya vyuo kama vile Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo Kikuu cha Dar es Saalam na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi.

Vingine ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Kikristo cha Tiba kilimanjaro(KCMUCo) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili(MUHAS).

"Kwa mfano kozi zote zinazotolewa na Muhimbili na nyingi za Chuo cha Ardhi zimejaa hadi sasa baadhi ya kozi zimekimbiliwa na waombaji wengi kuliko nafasi zilizopo katika vyuo vikuu hivyo," alisema.

Alizitaja baadhi ya kozi hizo kuwa ni ualimu, udaktari wa binadamu, ufamasia, uhandisi, Sayansi ya uthamini wa ardhi na sheria ambapo kwa kozi ya ualimu katika chuo kikuu kishiriki cha ualimu Dar es Saalam ilikuwa na waombaji 15,803 wakati nafasi zilikuwa ni 1,000 pekee.

Profesa Mwageni aliongeza kuwa kozi ya Sayansi ya Uthamini wa Ardhi ya Chuo Kikuu ilikuwa na waombaji 4,599 wakati nafasi ni 100, hata hivyo uchambuzi unaonesha kuwa waombaji wengi waliokosa nafasi katika vyuo ni ushindani uliopo kutokana na uhaba wa nafasi katika kozi hizo.

"Aidha baadhi ya waombaji hawakuzingatia sifa linganishi ambazo baadhi ya kozi hutaka wawe nazo ili wadahiliwe na kwamba kutokana na hali hiyo muda wa udahili umeongezwa kuanzia Septemba 12,mwaka huu hadi Septemba 23 na kwamba itakuwa fursa kwa waombaji ambao wana sifa wapte kuchagua tena kozi zenye nafasi stahiki," alisema.

Profesa Mwageni alisema waombaji hao walipaswa kuwa sifa za kuchagua kozi za masomo matano kulingana na sifa linganishi za kozi husika na kwamba kozi zingine humtaka mwombaji awe amefaulu somo au somo sio tu ya kidato cha sita bali pia ya kidato cha Nne.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: