Advertisement |
UJENZI wa Kiwanda cha saruji cha Dangote kimekamilika
kwa robo tatu na kinatarajia kuanza kazi ya uzalishaji Agosti, mwaka huu.
Kiwanda hicho kinamilikiwa na mfanyabiashara maarufu
nchini Nigeria, Alhaji Aliko Dangote kilichopo eneo la Msijute mkoani Mtwara, kina ukubwa wa hekta 2,971 na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha
tani 7,500 kwa siku na uzalishaji ukiongeza kwa mwaka watazalisha tani milioni
tatu.
Mwakilishi Mkazi wa kampuni hiyo nchini, Esther Kroll
alisema hayo alipozungumza na wajumbe wa Bodi ya Shirika la Petroli Tanzania
(TPDC), waliotembelea kiwanda hicho wakati wakifanya ziara mkoani hapa na
ujionea kazi za ujenzi zivyoendelea katika eneo hilo.
Esther alisema kikubwa hicho ni kikubwa Afrika ni kati ya viwanda 16 anavyomiliki mfanyabiashara huyo.
Alisema kukamilika kwa kiwanda hicho kinategemea
kuajiri wafanyakazi 10,000 ambapo watatoa kipaumbele kwa wananchi wa Mtwara
kuchangamkia fursa hiyo na ikionekana nafasi zingine zitakuwa wazi itawalazimua
watafute maeneo mengine.
Mwakilishi mkazi huyo alisema wiki mbili zijazo
wanatarajia kutangaza nafasi za kazi na watawapata wananchi wa Mtwara
watakaokuwa wanaomba kazi kupitia kwa wenyeviti kwani watakuwa wanawafahamu
wakazi wao.
Esther alisema kiwanda hicho ni kikubwa hivyo
kutakuwa na malori 600 yatakayokuwa yanasambaza saruji nchi nzima, pia
watatumia bandari, reli ya kati na TAZARA hivyo, watakuwa na wafanyakazi wengi.
“ Wapo makandarasi 1,200 ambao ni wazawa, Wachina 1,200 na Wahindi 20 wanaofanya kazi ya ujenzi katika kiwanda hiki kwa sasa,”alisema.
Alisema Alhaji Dangote wakati alipokuwa akiweka jiwe
la msingi Julai 27, mwaka 2012 aliahidi kutoa sh. milioni 450 kwa vijiji 10
vinavyozunguka eneo hilo kupitia Benki ya CRDB kupitia vikundi vyao vya Vicoba.
Pia, aliahidi kujenga soko la kisasa , kituo cha
polisi , hospitali na shule vyote vitajengwa wakati uzalishaji wa kiwanda
utakapoanza Agosti, mwaka huu.
Alisema kiwanda hicho kimejipanga kuanza kutoa fedha
hizo kwa vikundi mwezi ujao
na watatoza riba ndogo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Michael Mwanda, alipongeza kazi kubwa
inayofanywa ya ujenzi wa kiwanda na kwamba kitakapokamilika kitakuwa ni
mkombozi kwa wananchi wa Mtwara na wananchi wengine.
0 comments: