Friday, August 22, 2014

TMA wakutana na kamati ya Maafa

ad300
Advertisement
Washiriki wa Mkutano wa Jukwaa la Wadau wa Maafa (TANDREC).
JUKWAA la Kitaifa la Wadau wa Maafa (TANDREC), limependekeza kuendelea kutumika katika kubadilishana mawazo na watumiaji na watoaji wa huduma za hali ya hewa nchini.

Maamuzi hayo yalifikiwa jana, kwenye kikao cha pili cha mwaka cha kamati hiyo, kilichowakutanisha watendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Shirika la Hali ya Hewa Duniani na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Katika kikao hicho, pamoja na mambo mengine kwa kiasi kikubwa kilizungumzia utekelezaji wa GFCS hapa nchini ambapo hotuba ya ufunguzi, iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Florence Turuku, alielezea umuhimu wa utekelezaji wa GFCS na kazi za kamati ya Taifa kusimamia maendeleo yake.

Dk. Turuku alisema ni wazi kuwa upo umuhimu mkubwa wa kuhakikisha uwepo wa ushirikiano thabiti kati ya Kitengo cha Maafa nchini na GFCS ili kuleta tija kwenye shughuli za Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dk. Ellijah Mukhala, alieleza kuwa upo mpango wa utekelezaji wa GFCS, ambao kwa sasa umeanza kufanya kazi kwenye nchi za Tanzania na Malawi kwa udhamini wa serikali ya Norway na kutarajiwa kuenea katika nchi zingine miaka ijayo. 

Alisema mpango huo nchini Tanzania umeonyesha mafanikio makubwa kwa kipindi kifupi, kupitia timu ya Mradi inayoongozwa na TMA.

Mkutano huo wa wadau wa hali ya hewa ulijumuisha zaidi ya wadau 60 kutoka kwenye Taasisi za serikali, Taasisi zisizo za kiserikali na Wanahabari ambapo mapendekezo yote yalitolewa yalikuwa na lengo la kuboresha huduma za hali ya hewa.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: