Friday, August 22, 2014

Chama cha Kutetea Abiria Ubungo, chalalamika!

ad300
Advertisement
NDOTO ya viongozi wa Chama cha Kutetea Abiria kwenye kituo kikuu cha mabasi ya Mikoani na nchi jirani Ubungo (CHAKUA), imeonyesha dalili ya kuota mbawa kutokana na viongozi husika kurushiana mpira juu ya suala hilo.

CHAKUA walikua na ndoto ya kupewa ofisi ya kutekelezea majukumu yao katika eneo kilipo kituo hicho kwa sasa, baada ya ofisi yao ya awali kubomolewa katika mradi wa kujenga kituo kipya cha mabasi yaendayo kasi (DART).

Wakizungumza na blog hii Dar es Salaam jana, viongozi wa CHAKUA akiwemo Mwenyekiti Hassan Mchanjama, alisema wamefuatilia utaratibu wa kupewa ofisi hiyo mara kadhaa bila mafanikio.

Alisema kuwa walizingatia itifaki zote ikiwemo kupeleka maombi ya kiofisi kwa Meneja wa Kituo hicho cha Ubungo (UBT), ambaye aliwapa maelekezo ya kumuandikia barua Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam.

"Meneja alituambia tupeleke barua ya maombi kwa Mkurugenzi kule jiji kwakua yeye hana mamlaka ya kulitatua suala hilo. Tumeandika barua zaidi ya moja kwa vipindi tofauti bila majibu," alisema Mwenyekiti huyo.

Blog hii ilimtafuta Meneja wa Kituo hicho Kikuu cha Ubungo, Juma Idd, ambaye alikiri kuwa ni kweli aliwapa maelekezo hayo hivyo waendelee kusubiri.

Aidha aliongeza kuwa, baada ya bomboa bomoa taasisi nyingi zikiwemo za serikali zilizokuwa na ofisi kwenye majengo ya Kituo hicho, zimekosa kwenye kituo cha sasa cha muda hivyo CHAKUA kupatiwa ofisi ni jambo linalotia mashaka.

"Kuna taasisi nyingi za serikali zimekosa nafasi ya ofisi kwenye eneo tulilopewa na jiji sasa hivi. CHAKUA ni chama cha hiari, ila sijui ngoja tusubiri tuone, " alisema Meneja huyo.

Hata hivyo suala hili halikuishia hapo, gazeti hili lilifika ofisini kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, ambaye hakuwepo ofisini kwake, lakini ofisi ya Ofisa Uhusiano wa Halmashauri hiyo ilikiri kuwa barua za maombi ya CHAKUA hazijawafikia.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: