Advertisement |
Wakaanga Samaki, Soko la Ferry. |
Wito huo unakuja baada ya jitihada kadhaa wanazozifanya kupata nishati mbadala ya uhakika kugonga mwamba kutokana na njia hizo nyingi kutokuwa salama kwa afya na mazingira.
Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wakaanga Samaki soko la Ferry jijini Dar es Salaam (UWASA), Haji Mtulya, ni mmoja kati ya Wananchi hao ambao wameathirika na uhalisia wa nishati zilizoko hivi sasa.
Alisema kutokana na shughuli zao, wanatumia nishati ya kuni kukaangia samaki hali inayosababisha kupata matatizo ya kiafya kutokana na moshi pia kuharibu mazingira kwa namna moja au nyingine.
Kiongozi huyo alisema kwa kuliona hilo, Manispaa ya Ilala waliwapatia majiko yanayotumia nishati ya 'Sawdust' ambayo kutokana na kukosa ufanisi ikiwemo kutoa moto mdogo, wameamua kuyaacha na kurudi kwenye majiko ya kuni.
"Tulipewa majiko na Manispaa ili kuturahisishia kazi, kutulinda kiafya na kutunza mazingira, lakini hayana moto mkali na samaki wanahitaji moto mkali kweli kweli ili waweze kuiva vizuri. Hivyo tumeona turudi kwenye ya zamani kwani biashara ilishaanza kudorora," alisema.
Mtulya alisema baada ya kusikia juu ya kugundulika kwa gesi asilia nchini, katika juhudi zao za kuendelea kulinda mazingira walimtafuta Mtaalamu aliyebuni jiko la gesi ambalo wameshalijaribu na kuliona lina ufanisi wa hali ya juu.
Kwa mujibu wa wakaanga samaki hao, Jiko hilo limekubaliwa na Wanachama wote wa Umoja huo lakini kilio kilichopo ni juu ya bei ya gesi ambayo kiuhalisia ni ghali, hivyo mategemeo yote yamebaki kwa gesi asilia ambayo wamedai wamesikia itakuwa nafuu na yakutosha kwa Wananchi wote.
0 comments: