Monday, May 12, 2014

Wana CCM waambiwa umoja ni nguvu...

ad300
Advertisement
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kuachana na vitendo vya kutafuta wagombea wa nafasi mbalimbali kwa njia zisiyo rasmi kwasababu zinakinzana na katiba, kanuni ya chama hicho.

Pia wametahadharishwa kuwa viongozi wa chama hicho waliopo madarakani wako kwa mujibu wa sheria wakiwatumikia wananchi kwa uwezo wao wote, hivyo wanatakiwa kuwapa ushirikiano.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke, Yahya Sikunjema, alipokuwa akihutubia kwenye kikao cha halmashauri kuu maalum ya Kata ya Kigamboni.

Alisema amesikitishwa kusikia kuna baadhi wa watu wanafanya mchakato wa chini chini kuandaa viongozi  wanaodhani watawafaa hata kabla ya muda wa walioko madarakani kumalizika kwa mujibu wa katiba.

"Inasikitisha sana. Ni katiba pekee ya CCM (akiwa ameishikilia mkononi) inayoruhusu kuwepo kwa mkutano maalum wa kuteua mwakilishi wa chama kwa mujibu wa sheria. Kwanini kufanya kampeni za chini chini wakati hawa waliopo bado hawajamaliza muda wao, na wanafanya kazi vizuri huku nyie mkiwa ni mashahidi? Alihoji Sikunjema.

Mwenyekiti huyo alisema tabia hiyo ni mbaya na ni chanzo cha kutengeneza makundi kwenye chama tawala hatua inayofurahiwa na wapinzani.

Sikunjema aliwaambia wajumbe waliohudhuria kikao hicho kuwa wanatakiwa wawe wamoja kwa kushirikiana hatua kwa hatua kujenga chama kuanzia ngazi ya shina mpaka taifa.

Pia alikanusha uvumi uliokuwa umeenea miongoni mwa wajumbe kuhusu kutokuelewana kwa viongozi wa juu, Mbunge wa jimbo hilo Faustine Ndugulile, Diwani Dotto Msawa na yeye kuwa hazina ukweli.


Alisisitiza kuwa wanaoweza kukorofisha viongozi ni wajumbe wenyewe kwa kusambaza unafiki hali ambayo CCM haiikubali hivyo wenye tabia kama hizo waziache mara moja.

Sambamba na hayo aligusia kuwa baadhi ya viongozi wameanzisha taasisi za kusaidia wananchi kifedha (VICOBA), lakini ameshangazwa kuona kuwa kuna watu wanajitenga na  huduma za taasisi hizo kutokana na umiliki na kisha kulaumu viongozi kuwa hawawajali.

Katika kikao hicho kilichoandaliwa na Mwenyekiti huyo wa wilaya, alisema ataendelea na mpango huo wa kukutana na Wananchi kwasababu amegundua kuna taarifa ambazo huwa hazipati kwenye taarifa zinazofika ofisini kwake.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: