Monday, March 10, 2014

Watatu wapoteza maisha Dar!

ad300
Advertisement
WATU watatu wamepoteza maisha katika matukio matatu tofauti mkoani Dar es Salaam
likiwemo la Kamuru Hassan (32), mkazi wa Mbagala aliyekutwa amejinyonga ndani ya chumba
chake.

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Temeke Englebert Kiondo alisema juzi majira ya saa 9
alasiri katika eneo la Mbagala, jeshi lake limemkuta mtu huyo akiwa amejinyonga kwa waya
kwenye paa la nyumba.

Alisema mwili wa mtu huyo aliyetambuliwa kwa jina la Kamuru Hassan (32), ulikutwa
umening'inia ndani ya chumba lakini sababu ya kujinyonga haijafahamika kutokana na mtu
huyo kutoacha ujumbe wowote.

Kamanda Kiondo alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ya Temeke kwa
uchunguzi zaidi.

Katika matukio mengine, Jeshi la polisi mkoa wa kipolisi wa Ilala limemkuta mwanaume
aliyetambuliwa kwa jina moja la Njegera anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 50 na 55 akiwa
amekufa katika eneo la Upanga.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Marietha Minangi amesema mwili
huo ulikutwa katika eneo la Senegal, Upanga juzi majira ya saa kumi na mbili na nusu jioni.

Kamanda Marietha alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakazi wa eneo hilo, mtu huyo
alikuwa akiishi maeneo hayo kwa miaka mingi.

Anasema kutokana na uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi, hakukuonekana jeraha lolote
katika mwili huo hivyo wameupeleka katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi
huku jeshi la Polisi likiendelea na upelelezi juu ya tukio hilo.

Na tukio la mwisho lilimuhusisha mtu aliyetambulika kwa jina moja ya Mjomba anayekadiriwa
kuwa na miaka 35 mpaka 40 mkazi wa Mlalakuwa, Kinondoni aliyekutwa amekufa kwenye kituo
cha mabasi cha Mwenge.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema mwili wa mtu huyo
aliyekuwa akifanya shughuli za kuokota chupa za plastiki umekutwa juzi katika eneo hilo majira
ya saa 9 alasiri.

Alisema mwili huo umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi zaidi
na utambuzi.

Kamanda huyo alisema jeshi la polisi halijajua sababu ya kifo hicho kutokana na kukosekana
kwa majeraha katika mwili wa marehemu, lakini upelelezi bado unaendelea.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: