Monday, March 24, 2014

TMA yafikia kilele siku ya Hali ya Hewa duniani kwa kuwafunda vijana.

ad300
Advertisement
VIJANA wamehimizwa kufuatilia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) ili wapate ufahamu juu ya namna ya kupambana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa katika kujipatia maendeleo kiuchumi.

Wito huo ulitolewa jana na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) , Agnes Kijazi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya hali ya hewa duniani.

Agnes alisema Machi 23 kila mwaka ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Shirika la hali ya hewa duniani (WMO), ambalo lilianzishwa 1950 nchini Uswisi, maadhimisho ambayo yalianza Machi 21 na kufika kilele chake Machi 24.

Alisema kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni 'Ushirikishwaji wa Vijana katika Masuala ya Hali ya Hewa' kauli ambayo imemlenga kijana popote alipo duniani kuchukua hatua za awali kupambana na vitendo vya uharibifu wa mazingira unaochangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la joto.

Kwa mujibu wa Agnes, katika kushiriki maadhimisho hayo TMA ilitembelea shule na vyuo mbalimbali nchini ili kuwafikia vijana na kuwapa elimu juu ya hali ya hewa na umuhimu wake katika mustakabali wa maisha yao, zoezi ambalo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mkurugenzi huyo wa TMA alisema hatua ya WMO  ya kuwashirikisha vijana katika masuala ya hali ya hewa ni muhimu kwa ustawi wa kizazi hiki na kijacho ili kujenga jamii imara hapo baadae, hivyo kijana wa Kitanzania alizingatie hilo.

Pia alisema kitendo cha Shirika la Hali ya Hewa kuwahamasisha vijana ulimwenguni ili kujihusisha na masuala ya hali ya hewa ili kupata maarifa na uelewa wa hatua za kuchukua katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa, wao kama TMA watalifanya kuwa zoezi endelevu.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: