Monday, March 24, 2014

Mwenyekiti CCM Ilala awaasa Watanzania

ad300
Advertisement

WATANZANIA wametakiwa kushirikiana kwa kuweka kando itikadi za vyama vyao vya Siasa wakati wa jukumu la kupitisha muundo wa serikali utakaotambuliwa na katiba mpya ya nchi mara watakapotakiwa kufanya hivyo.

Imeelezwa kuwa rasimu ya katiba inayofanyiwa kazi na wajumbe wa bunge maalum la katiba mjini Dodoma imependekeza muundo wa Serikali tatu, ambao hauna tija kwa maendeleo, umoja na mshikamano wa taifa.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya IIala ambaye pia ni  diwani wa kata ya Vingunguti Asaa Simba alipokutana na Umoja wa wanawake (UWT), kata ya Vingunguti tawi la Mtambani.

Asaa Simba - Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala.
Alisema ni wazi kuwa muundo wa Serikali unaofaa kwa usalama na maendeleo endelevu ya nchi ni ule uliopendekezwa na Halmashauri kuu ya chama tawala CCM wa Serikali mbili na si vinginevyo.

Mwenyekiti huyo wa wilaya aliwaambia Wanawake waliohudhuria mkutano huo kuwa, wao ni mhimili mkubwa wa Chama katika ushindi wa chaguzi mbalimbali hivyo waungane na kuwaeleza wengine wasio Wanachama umuhimu wa Serikali mbili ili hatimaye maoni ya wananchi yaweze kuamua juu ya hilo.

Alisema muundo wa Serikali tatu ni mzigo kwa taifa katika uendeshaji na ni wazi kuwa wanaouunga mkono ni wale wenye uchu wa madaraka ambao mwisho wake husababisha kusambaratika kwa Serikali kutokana na kutotawalika.

Asaa aliwaambia wanachama hao wa UWT kuwa wasisikilize maneno ya Wachache wanaodhani kuwepo kwa serikali tatu ni jibu la kero kadhaa zilizopo, kwasababu kamwe si suluhisho na kero hizo zinatatulika kwa kutumia muundo wa Serikali mbili kadri muda na fedha kutoka Serikali kuu na wahisani zitakaporuhusu.

Pia alitumia nafasi hiyo kuwataka Wakinamama wenye nia na uwezo wa kushika nafasi ya uongozi kwenye ngazi ya Serikali za mitaa, kujitokeza kugombea nafasi hizo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyia Oktoba mwaka huu.

Aidha Diwani huyo alisema Serikali kutokana na ukubwa wa kata ya Vingunguti, imeamua kuigawa mitaa iwe Mtambani na Faru ambapo pia kutakuwa na kata mpya iitwayo Mnyamani ili Wananchi wapate huduma za kijamii kulingana na idadi yao ndogo bila msongamano mkubwa.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: