Tuesday, March 25, 2014

John Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Mara, afariki dunia

ad300
Advertisement
John Tupa enzi za Uhai wake.
MKUU wa mkoa wa Mara John Tupa amefariki dunia wakati akielekea kufunga mafunzo ya mgambo kwenye kituo cha Nyamawale wilayani Tarime mkoani humo.

Habari za kuaminika zilisema Mkuu huyo wa Mkoa alianguka ghafla na kupoteza fahamu huku povu likimtoka mdomoni saa 4.00 leo asubuhi katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime John Henjewele.

Kabla ya tukio hilo Tupa alikuwa kwenye kikao pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Mara ili kujiandaa kuanza ziara mkoani humo, ambapo alitakiwa kufunga mafunzo ya Mgambo yaliyowajumuisha vijana zaidi ya 100 kutoka pembezoni mwa mgodi wa North Mara.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya Mkuu huyo wa mkoa kuanguka aliwahishwa hospitali ya Wilaya Tarime kwa ajili ya matibabu lakini mara tu baada ya kuwasili Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Michael Negga alithibitisha kifo chake.

Mganga huyo wa Wilaya alisema baada ya uchunguzi wa kitaalamu ilionekana kuwa kifo hicho kimesababishwa na shinikizo la damu pamoja na kisukari.

Mwili wa Marehemu ulipelekwa Musoma kuhifadhiwa huku taratibu za maandalizi ya shughuli za Mazishi ya kiserikali zikisubiriwa.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: