Monday, March 24, 2014

Serikali yaipatia kinondoni gari la wagonjwa

ad300
Advertisement
Mwenyekiti wa bodi za Afya mkoa wa Dar es Salaam Jerome Ringo (kushoto) akimkabidhi funguo wa gari jipya la kubebea wagonjwa Meya wa Kinondoni Yusuph Mwenda


Meya Mwenda akitoka kwenye gari mpya ya wagonjwa mara baada ya kuizindua
SERIKALI ikishirikiana na benki ya taifa ya biashara(NBC), imeikabidhi Manispaa ya Kinondoni gari la kubebea wagonjwa lenye thamani ya sh. milioni 90 ili kurahisisha utoaji huduma za afya hususan katika maeneo ya pembezoni.

Gari hiyo na. T 932 CJS aina ya NISSAN imekabidhiwa jana kwa Meya Yusuph Mwenda na Mwenyekiti wa bodi za afya mkoa wa Dar es Salaam Jerome Ringo aliye mwakilisha Rais Kikwete.

Katika makabidhiano hayo, Meya Mwenda alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Kikwete kwa kuiona Manispaa yake na kwamba atahakikisha linatumika kama ilivyokusudiwa.

Pia alisema anawashukuru viongozi wa benki ya NBC, ambayo imeshirikiana na Serikali kwa muda mrefu sasa katika kuiinua sekta ya afya nchini.

Aidha kwa upande wa Mwenyekiti wa bodi za afya, Jerome Ringo alisema Rais alichagua kuipatia Manispaa ya Kinondoni kwakua ina changamoto kubwa kwenye utoaji wa huduma za afya kutokana na ukubwa wake.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Manispaa hiyo Dk. Gunini Kamba, alisema gari hilo limekuja wakati muafaka ambapo wamevalia njuga utoaji wa huduma za afya sehemu za pembezoni ikiwemo maeneo ya Mabwepande na Bunju.

Aliongeza kuwa kuwasili kwa gari hilo, kutawafanya watumie gari iliyopo kuwahudumia wanawake na watoto huku hili jipya likihudumia wanafunzi katika shule zote za Manispaa ya Kinondoni.

Sambamba na gari hilo, pia vilitolewa vifaa vya maabara iliyopo ndani ya gari hilo vyenye thamani ya sh. milioni 20 ambavyo vimejumuisha hadubini na mashine nyingine za upimaji wa magonjwa.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: