Friday, February 7, 2014

Zaidi ya Bilioni 17 zatarajiwa kukusanywa Dar 2014/2015.

ad300
Advertisement

HALMASHAURI ya jiji la Dar es Salaam inakusudia kukusanya zaidi ya sh. bilioni 17 kwa mwaka ujao wa fedha kwa ajili ya matumizi ya ndani na miradi ya maendeleo.

Vyanzo vya mapato hayo vinatarajiwa kuwa ni ushuru wa ndani  wa sh. 9,902,022,451 wakati sh. 7,262,048,400 zikitarajiwa kutoka serikali kuu na kwenye miradi ya maendeleo.

Hili limekuja baada ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji hilo kupitisha kwa pamoja rasimu ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha, kwenye kikao kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa mkutano wa Karimjee.

Meya wa jiji Mstahiki Dk. Didas Masaburi, amesema kuwa dira ya jiji hilo ni kuwa na mafanikio endelevu, huduma bora na mazingira yanayovutia uwekezaji kwa kutegemea rasilimali zilizopo ili kupunguza umasikini na kukuza uchumi.






Amesema miongoni mwa maeneo waliyokubaliana na baraza la Madiwani la halmashauri ya jiji kuyapa kipaumbele kwenye bajeti hiyo, ni pamoja na dira ya maendeleo ya kitaifa, MKUKUTA pamoja na ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015.

Dk. Massaburi alieleza kuwa kwa mwaka uliopita wa fedha, Halmashauri ilikadiria kukusanya kiasi cha zaidi ya sh. bilioni 13 kutokana na vyanzo vya ndani na ruzuku kutoka Serikali kuu pamoja na mkopo wa Taasisi za fedha.

Aidha alitaja miradi ya maendeleo ambayo Halmashauri hiyo imepanga kuitekeleza kwenye bajeti iliyopitishwa jana, kuwa ni uendelezaji wa viwanja na maeneo mapya kwa ajili ya dampo la kisasa, machinjio na uwekezaji.

Pamoja na hayo, wanatarajia kujenga ukuta wa kuzunguka dampo la Pugu Kinyamwezi, ujenzi wa bwawa la maji machafu, ukarabati wa majengo ya Halmashauri ikiwemo jengo la Karimjee na Mahakama ya jiji pamoja na udhibiti wa virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao hicho, Mbunge wa Kinondoni (CCM), Iddi Azzan ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri ya jiji alisema ni bajeti nzuri iliyopitishwa kwa wakati muafaka ikizingatia mahitaji ya wananchi wengi wa Manispaa zote tatu za jiji.

"Nimeunga mkono mswada kwani ni bajeti nzuri, inamjali Mwananchi wa Manispaa zote za jiji kwenye sekta karibu zote, kwahiyo itekelezwe kwa mujibu wa kanuni kama tulivyokubaliana," alisema Mbunge huyo wa jimbo la Kinondoni.



Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: