Friday, February 7, 2014

Akutwa amekufa ndani ya basi Dar..

ad300
Advertisement
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Camilius Wambura
CHRISTINA Maziku (47), mwenyeji wa Uzinza Geita amekutwa amekufa akiwa amekaa kwenye kiti cha basi eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura  amesema mtu huyo amekutwa jana kwenye kituo cha mabasi yaendayo mkoani, akiwa ndani ya Basi la kampuni ya Lushanga express inayofanya safari zake kutoka Dar kwenda Geita.

Amesema Christina alikuwa amemleta Kaka yake Shija Maziku (49), mwenye tatizo la kansa ya ngozi kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya Ocean road iliyopo jijini Dar es Salaam.

Kamanda Wambura amesema taarifa kutoka kwa Kaka wa marehemu, Shija, zilieleza Christina enzi za uhai wake alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu kwa kipindi cha muda mrefu.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili (MNH)na Jeshi la polisi limesema upelelezi zaidi juu ya tukio hilo unaendelea.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: