Tuesday, February 4, 2014

Tanzania Revenue Authority (TRA)

ad300
Advertisement
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), wamedhamiria kuendelea kukusanya Mapato ya Serikali kwa urahisi na uwazi bila kumpa wakati mgumu mlipakodi.

Dhamira hiyo imetolewa na Mamlaka hiyo kwenye Muhtasari wa Mpango Mkakati wa Nne kama lengo waliojiwekea mpaka kufikia mwaka wa fedha 2017/2018.

Kutokana na hili, baadhi ya Wafanyabiashara waliiambia Blog hii kuwa kama Taasisi ya Serikali yenye jukumu zito kwa Maendeleo ya Taifa ni hatua nzuri iliyochukua kwa kuanzia kuelekea kwenye lengo kuu.

"Wanaweza, sema wakuu wa Taasisi hii wanatakiwa kuhakikisha watendaji wanazingatia maadili ya Kazi, wasipende kula Rushwa, wakizingatia hilo malengo yao watayafikia," alisema Feysal Mohamed mmoja wafanyabiashara wa vifaa vya Elektroniksi katikati ya Jiji.

Naye Meneja wa kitengo cha Elimu kwa Mlipakodi (TRA) Makao Makuu Diana Masalla, alieleza kuwa TRA wanafanya kila waliwezalo kuhakikisha wanamjali mteja kwa kumpatia anacho kihitaji kwenye huduma.

Alieleza kuwa umefika wakati, Mwananchi atambue mchango wao katika mafanikio yake kibiashara na Maisha yake kiujumla kwani kwa kufanya hivyo hata jaribu kukwepa ulipaji wa kodi kwa kujua umuhimu wa kufanya hivyo.

Aidha, TRA ilisema mikakati yake inaitekeleza kwa kuzingatia mihimili mitatu ambayo ni Urahisi, Uhiari na Uboreshaji endelevu yenye lengo la kupata mawazo ya kimkakati ya kuijenga Taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.      
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: