Tuesday, February 4, 2014

BAR Zafungwa!!

ad300
Advertisement
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imezifungia baa 15 zilizopo kwenye kata ya Kunduchi, Makongo na Bunju.

Baa hizo zilizofungiwa ni Ngalawa, Malanja, Madrid, Y2K, Resort , Patamu beach, Edge, Wakongwe, Noel pub , Bondeni pub, Jueva, Sitting room, Esk Green Park, Magoma moto  na Lina park.

Afisa Biashara wa Mansipaa hiyo Ananias Kamundu, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.

Alisema sababu za kuzifungia baa hizo ni wamiliki kukiuka masharti ya leseni ya biashara husika.

"Tuliwapa leseni zikiwa na masharti kadhaa. Muda wa  kufungua na kufunga baa, ni moja ya masharti hayo. Imejieleza wazi kuwa wanatakiwa kufungua baa zao saa 12 jioni na kufunga saa tano usiku, lakini wamekuwa wakienda kinyume na masharti hayo,"alisema.

Afisa Biashara huyo alisema wamekuwa na desturi za kupiga muziki kwa sauti kubwa, hali inayopelekea kuwa kero kwa wakazi waliokaribu na maeneo ya baa hizo.

Aidha alibainisha kuwa kufungiwa kwa baa hizo kumetokana na malalamiko yaliyopelekwa na wananchi kwenye manispaa hiyo kwa kupitia viongozi wao wa Serikali za Mtaa.

"Hatujawanyang'anya moja kwa moja leseni zao, wanachotakiwa kufanya ni kuandika barua ya kukiri makosa yao na kuahidi kutorudia tena nasi hatutosiota kuwarudishia,"alisema.

Pia alisema wanakabiliwa na  changamoto ya kuzuia wamiliki wa baa kufunga baa zao muda husika, kutokana na wamiliki hao kudai kuwa asubuhi hawauzi vileo zaidi wanauza supu.

Afisa huyo aliongeza kuwa wanapozikuta baa zikitoa huduma ya vileo muda ambao upo kinyume na masharti ya leseni wanazitoza faini  ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.

Sanjari na hayo, alisema kwa kuwa zoezi hilo ni endelevu, na alilitaka Jeshi la Polisi kushirikiana na Manispaa hiyo katika kusimamia utekelezaji wa Sheria wanazozitoa, ikiwemo kuhakikisha baa walizozifungia haziendelei na biashara husika mpaka watakapo ruhusiwa tena na Manispaa hiyo.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

1 comment:

  1. asante sana kaka , kazi nzuri , big up , na mungu akubariki sana...
    kama kweli hii umeandika mwenyewe nakupa sifa sana bwana willy
    mimi NORMAN

    ReplyDelete