Wednesday, February 12, 2014

Serikali yaokoa jahazi la Elimu Ilala.

ad300
Advertisement
SERIKALI inaendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa 67 katika manispaa ya Ilala ili kupunguza idadi ya wanafunzi waliokosa nafasi za kidato cha kwanza kwenye shule hizo.

Vyumba hivyo vya madarasa  vimejengwa kwenye shule kumi za manispaa hiyo na viko katika hatua za mwisho kukamilika.

Akizungumza na blog hii ofisini kwake jana, Afisa elimu wa sekondari manispaa ya Ilala, Violet Mlowosa, alisema hatua hiyo imechukuliwa na serikali kwa haraka ili kuwasaidia wanafunzi kupata haki yao ya msingi ya elimu kwenye shule walizochaguliwa.

Alizitaja shule hizo za Sekondari kuwa ni Mchanganyiko, Binti Mussa, Juhudi, Pugu stesheni, Majani ya chai, Ulongoni, shule ya sekondari Magoza, Ugombolwa, Zawadi na Msimbazi.

Alisema ujenzi huo umezingatia uwepo wa eneo kwenye shule husika na uhitaji kutokana na idadi ya Wanafunzi wasio na madarasa yakuridhisha kusomea bila usumbufu.

Afisa huyo alisema utaratibu huo ni endelevu kwa mujibu wa Serikali kuu, mpaka watakapohakikisha wamelitatua tatizo la uhaba wa madarasa kwenye shule nyingi za Sekondari.

Alieleza kuwa changamoto inayoikabili Manispaa hiyo kwenye taaluma ni walimu wa masomo ya sayansi hususani masomo ya Physics, Chemistry na Hesabu na kukiri ni tatizo la kitaifa lakini aliomba itafutwe njia mbadala  ya kulitatua hilo.

Violet alisema, vitabu kwenye shule za sekondari manispaa ya Ilala sio tatizo kwani Serikali imejitahidi kukabiliana na hilo kwa kutoa fungu hazina, maalum kwa ununuzi wa vitabu shuleni.

Aidha Afisa huyo aliwataka wazazi kutoa kipaumbele kwenye elimu ya watoto kwa kubainisha kuwa elimu si jukumu la serikali tu bali mzazi naye anahusika kwenye maendeleo ya sekta hiyo kwa kuchangia michango michache iliyopo shuleni kama vile ya chakula cha mchana kwa ajili ya mtoto.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: