Thursday, February 13, 2014

Dampo la jiji Dar, MAJANGA.

ad300
Advertisement
DAMPO la jiji la Dar es Salaam limesemekana kuwa ndio kikwazo kikubwa cha mapambano ya kuliweka jiji safi kwa muda mrefu sasa.

Dampo hilo lililopo Manispaa ya Ilala eneo la Kinyamwenzi nje kidogo ya jiji limelalamikiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni binafsi zilizopewa jukumu la kusafirisha uchafu kutoka katikati ya mji.

Meneja wa oparesheni kampuni ya Green Waste Pro, Abdallah Mbena aliiambia blog hii jana, kuwa hali ya dampo la jiji si rafiki kwa utendaji wao wa kazi kwani inaharibu sana vitendea kazi vyao yakiwemo magari ya kisasa yaliyoingizwa nchini miaka michache iliyopita yakiwa mapya.

Alieleza kuwa magari hayo ya kubebea taka kwenye kampuni yao, yameshachoka wakati hayana hata miaka miwili kwenye kazi kutokana na ubovu wa miundombinu wanayokutana nayo dampo.

"Kipindi cha kiangazi ukienda dampo, gari inaingia kwenye uchafu karibu tairi zote zinapotea, ni tope hasa na kutoka hapo huwa inakuwa shughuli mpaka kuvutwa, sasa fikiria kipindi cha mvua hali inakuwaje? kweli Serikali iliangalie hili," alisema Mbena.

Alisema kampuni yao inajizatiti kutoa huduma kwa mujibu wa mkataba wao, lakini hali ni ngumu mno kwani kuachilia mbali ubovu wa miundombinu hususani dampo, wananchi ambao ndio wateja wao wamekuwa wakikwepa kulipia huduma ya kukusanyiwa taka majumbani mwao hali inayoongeza ugumu wa kazi yao.

Mbena alisema katika kulidhibiti hilo, wameshirikiana kwa karibu na Manispaa ya Ilala na baadhi ya Wananchi katika kuwakamata wote wanaokwenda kinyume na makubaliano yao kisha huwapeleka mahakamani au kuwatoka faini kwa mujibu wa makubaliano.

Aliitaka zaidi Serikali iipe uzito jitihada zinazofanywa na wachache wa kuliweka jiji safi hususani     Manispaa ya Ilala ambayo ndiyo sura ya mkoa, kwa kuwekeza zaidi kwenye usafi kama kutenga eneo la wazi maalum kwa wananchi kukusanya uchafu.

Eneo hilo litarahisisha kazi ya wanaokusanya uchafu kuweza kufanya kazi hiyo kwa haraka kwani kuna baadhi ya mitaa katikati ya jiji haifikiki kirahisi na gari za kuzolea taka kutokana na kuwepo kwa maegesho ya magari yasiyo rasmi pande zote za barabara.

Aidha, alibainisha kuwa elimu kwa wananchi juu ya usafi na jinsi uchafu unavyoweza kuwa na manufaa kwao kwa kutengenezea kitu kingine mfano mbolea, inahitajika zaidi kutokana na hali halisi inavyoonekana kuwa watu hawana elimu ya namna hiyo, pamoja na ile ya utunzaji wa mazingira kwa ujumla,

Meneja huyo alisema miundombinu ya barabara jijini Dar es Salaam inatakiwa iangaliwe kwa jicho la tatu ili kupunguza baadhi ya kero zilizopo hivi sasa ikiwemo foleni kwani kwenye kazi zao, hilo linawakwamisha sana katika kufanya kazi kwa uharaka.

Alishauri Serikali kupitia idara husika iweke msimamo barabara za akiba zisitumiwe na magari binafsi na badala yake yapite magari ya taka, kubebea wagonjwa, zimamoto na yenye dharura za namna hiyo.   
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: