Tuesday, February 18, 2014

Kinondoni yapania kufikia 100% katika ukusanyaji Kodi.

ad300
Advertisement
ZAIDI ya bilioni 100 zinatarajiwa kukusanywa na Halmashauri ya Kinondoni katika mwaka wa fedha 2014/2015 kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za Manispaa hiyo.

Kati ya hizo bilioni 78 zitatoka Serikali kuu, zaidi ya bilioni 6 ruzuku kutoka TAMISEMI huku kiasi cha 37,427,797,677 kikitegemewa kukusanywa kwenye mapato ndani ya Kinondoni.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa Baraza la Madiwani kwenye ukumbi wa mikutano wa Manispaa hiyo mwishoni mwa wiki, Mstahiki Meya wa Kinondoni Yusufu Mwenda, alisema mafanikio waliyoyapata kutokana na ukusanyaji wa mapato ndani ya Manispaa kwa mwaka wa fedha unaoishia ni kubwa na inastahili pongezi.

Alisema makadirio ya kukusanya fedha za ndani waliyoyapanga kwenye bajeti ijayo ni 30.5% ya bajeti yote kwasababu ya ongezeko la sh. bilioni 8 hivyo itapunguza utegemezi kwa serikali kuu kwa kiasi fulani kulinganisha na mwaka uliopita.

Mstahiki Meya alisema makadirio ya ongezeko la bilioni 8 kwa mwaka ujao wa fedha unatokana na Halmashauri hiyo kuanza kukusanya kodi ya leseni za bishara na majengo, ambazo hazikuwa zikikusanywa katika miaka iliyopita.

"Mwaka wa fedha uliopita tulikuwa na uwezo wa kukusanya 27% tu ndani ya Halmashauri yetu, lakini sasa kutokana na juhudi zetu tumefikia 30%, nawaomba tushirikiane tuongeze juhudi kwenye ukusanyaji wa fedha za ndani ili kujihakikishia uwezo wa kuendesha halmashauri pamoja na miradi yetu ya maendeleo," alisema Meya Yusufu.

Aidha alisema kupitia bajeti hiyo Halmashauri imejizatiti kutekeleza malengo ya MKUKUTA, Ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi (CCM), ambayo inasisitiza kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa vijana kwa nia ya kupunguza umasikini wa kipato.

Pia Mstahiki Meya alisema katika mwaka wa fedha 2014/2015 kama ilivyokuwa kwenye bajeti ya 2013/2014, halmashauri hiyo itaendelea kutekeleza malengo ya Milenia na dira ya taifa ya maendeleo ya 2025.

Aliwataka Wananchi watambue kuwa Halmashauri ni chombo chao kilichopo kisheria kwa ajili ya kushirikiana na mwananchi katika uzalishaji kwa kutumia fursa zilizopo ili kujiletea maisha bora.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: