Advertisement |
Msongamano wa magari na matumuzi ya barabara za akiba usiozingatia kanuni na taratibu ni tatizo lingine kutokana na vyombo vya uokoaji kushindwa kupita kwa urahisi kwenda maeneo ya matukio
Haya yameelezwa jana na Kaimu Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Ilala, Mabusi Peter wakati akizungumza na Uhuru katika mahojiano maalumu, ambapo alisema wamekuwa wakielekezewa lawama nyingi kutoka kwa wananchi licha ya kuwepo changamoto hizo.
Alisema Kikosi cha Zimamoto kinajitahidi kwa kiasi kikubwa kutekeleza majukumu yake licha ya changamoto hizo na kwamba, hata miundombinu ya upatikanaji ya maji imekuwa na changamoto kubwa hatua inayosababisha wakati mwingine kufika eneo la tukio bila kuwa na maji ya kutosha..
Hata hivyo, alisema kuwa madai kuwa magari ya zimamoto yamekuwa yakienda eneo la tukio bila maji hayana ukweli na kuwa hubeba maji kulingana na ujazo wa gari husika
Alisema wanajitahidi kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na kuwahi kutoa taarifa kwao mara tu moto unapoanza kwa kupiga simu ya bure namba 114 na si kufanya hivyo mpaka moto unapowazidi nguvu.
Aliongeza kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kuwa na vifaa vya tahadhari vya kuzimia moto nyumbani, ikiwemo mitungu midogo ya gesi na ndoo cha mchanga.
Aliwaahidi watanzania kuwa maboresho makubwa yanakuja katika siku za karibuni kwa kuwa Kampuni ya Ujenzi wa Barabara ya STRABAG, imejenga visima zaidi ya 50 vya maji ambayo yatatumiwa na zimamoto katika njia za Mradi wa Mabasi yaendayo haraka.
0 comments: