Wednesday, January 22, 2014

Watanzania waula CAF

ad300
Advertisement
SHIRIKISHO la mpira wa Miguu Afrika CAF, limewapa ulaji makamishna wawili wa Tanzania .

Makamishna hao ni Lina Kessy ambaye amepata ulaji wa kuchezesha mechi ya ligi ya mabingwa Afrika kwa wanawake kati ya Kenya na Rwanda mchezo utakaofanyika Rwanda Februari mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF, Boniface Wambura alisema mbali na Lina pia Alfred Luiza amechaguliwa kuchezesha mechi ya kombe la mabingwa Afrika.

Wambura alisema uteuzi huo umeifanya TFF kufarijika na kuona watanzania nao wanapata nafasi za kuchezesha mechi kubwa kama hizo.

Wambura alisema Luiza atachezesha mechi   kati ya Shelisheli na Angola ambayo pia itachezwa Shelisheli Fbruari mwaka huu.

Wakati huo huo TFF imesikitishwa na kifo cha mchezaji wa Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars Angela Kajanja aliyefariki Dunia jana.

Angela alikuwa ni mchezaji  wa timu ya Twiga Stars na alikuwa akiichezea timu ya wanawake ya Sayari.

Wambura alisema kifo cha mchezaji huyo ni pigo kwa wanasoka hususani wachezaji wa timu ya Twiga Stars ambao walikuwa wakicheza nae katika kikosi hicho.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: