Tuesday, January 21, 2014

Wizi wa Mil. 30 wampeleka Kizimbani

ad300
Advertisement
MAHAKAMA ya wilaya Ilala chini ya Hakimu Janeth Kinyange imewapandisha Kizimbani watu watatu wote wakazi wa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za wizi wa gari lenye thamani ya sh. million 30.

Isack Mwakatobe(32), ambaye ni dereva, Marius Donasius(40) fundi makenika, pamoja na Hamadi Athumani(34), wametuhumiwa kuhusika na wizi huo wa gari aina ya Toyota DCM lenye namba za usajili T361ADH mali ya Atish Bagwanji.

Akiwasomea shtaka hilo, wakili wa serikali Cecilia Mkonongo, alisema watuhumiwa hao walifanya kosa hilo siku ya tarehe 31 oktoba mwaka jana kwenye kituo cha kuuzia mafuta cha OPEL kilichopo Fire jijini Dar.

Washtakiwa wote wamekana shutuma hizo na kuamuriwa na mahakama kwa mujibu wa sheria na. 148 kifungu kidogo cha 5(e), kuwasilisha mahakamani hapo wadhamini wawili wenye kazi za kudumu na barua ya muajiri, sambamba na fedha taslimu sh. milioni tano au hati ya mali siyo hamishika yenye thamani sawa na fedha tajwa.

Hakimu Kinyange aliahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 30 mwezi huu, na kuamuru watuhumiwa wote kurudishwa rumande. 
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: