Advertisement |
Malalamiko hayo yametokea baada ya magari hayo yanayomilikiwa na Manispaa zilizopo hapa jijini, kuharibika barabarani mara kwa mara hali inayoleta usumbufu kwa wakazi pamoja na watumiaji wa barabara.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema magari hayo yanaonekana ni ya muda mrefu na yamekosa uangalizi wa mara kwa mara wa kiufundi ambayo yatayawezesha kufanya kazi ipasavyo na kupunguza kuharibika mara kwa mara.
Akizungumza na blog hii mkazi wa Pugu Kajiungeni, Vincent Leonard alisema mara nyingi gari za taka zinazima katikati ya barabara kwa siku mbili hadi tatu, ndipo linapotokea lingine kupakua uchafu kupeleka dampo huku lile la awali likiachwa pale pale.
Leonard alisema, hali hiyo inasababisha mazingira kuwa machafu pamoja na hali ya hewa kuwa mbaya hivyo kusababisha uwezekano wa kutokea kwa magonjwa mbalimbali ya mlipuko.
Naye mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Rehema Chuwa mkazi wa Kinyamwezi dampo alisema kuwa magari hayo ya taka kwa muonekano yako kama takataka kutokana na hali ya uchakavu yaliyokuwa nayo.
"Ukiyakuta yamesimama dampo pale huwezi hata kuamini kuwa yameleta taka na yanarudi mjini, yapo kama takataka, kweli wahusika waliangalie suala hili kwa jicho la tatu", alisema Rehema.
0 comments: