Tuesday, January 21, 2014

Wananchi wakishukia Kikosi cha Usalama Barabarani

ad300
Advertisement
JESHI la polisi kikosi cha usalama barabarani limeshauriwa kuhakikisha linasimamia utelekezwaji wa sheria kikamilifu, kama suluhisho mojawapo la kupunguza ongezeko la ajali za barabarani zitokanazo na uzembe hususani zile za pikipiki.

    Hatua hiyo imeelezwa kuwa muarobaini wa mabadiliko kwa watumiaji wa barabara wakilengwa zaidi wanaotumia vyombo vya moto vikiwemo pikipiki, bajaji na magari ambao wamekuwa wakivunja sheria za barabarani mara kwa mara, jambo linalo wasababishia ajali zinazo poteza maisha ya watu wasio na hatia.

    Changamoto hiyo imetolewa na baadhi ya wakazi wa eneo lililopo nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam la Chanika, Manispaa ya Ilala ambao wamelaumu jeshi la Polisi kwa kile walichokiita ‘kulisahau’ eneo hilo katika suala la utelekezaji wa sheria bila shuruti japo kuna kituo kidogo cha Polisi katika eneo hilo.
    “Kweli ninaona kituo cha hapa Chanika kipo kama kipo tu, pikipiki zinabeba watu wanne mpaka watano kwa mara moja (Mshikaki) zinapita mbele ya kituo kwenda Masaki na askari wapo tu wanaangalia na wanakua hawajavaa helmet wala nini” alisema Mkazi aliyejitambulisha kwa jina la Mustapha Ally.
    Alisema suala la usimamiaji wa sheria linatakiwa litiliwe mkazo kuliko ilivyo sasa, pikipiki moja ipakie watu wawili huku wote abiria na dereva wake wavae kofia za usalama (helmet) ili kuwasaidia mara inapotokea ajali.
    “Zile helmet zinasaidia kweli, polisi wasimamie hili, maisha ya watu yanapotea sana kwa ajali za pikipiki kila sehemu Tanzania tunasikia, ila Chanika hebu wafanye operesheni ya mfano ya uvaaji wa helmet na ubebaji wa abiria idadi inayo takiwa kwenye pikipiki, na madereva bodaboda waache tamaa ya hela ya haraka haraka.” 
    Naye Hamisi Sultan (34), ambaye ni Mkazi wa eneo la Chanika Magengeni amesema jeshi la Polisi wa usalama barabarani limeonekana kutilia mkazo sana maeneo yaliyopo karibu na katikati ya jiji la Dar Es Salaam na kuacha maeneo ya kando ya jiji yakiwa hayana uangalizi wao wa karibu mpaka linapo tokea la kutokea mfano ajali ndipo wanapigiwa simu na kuja kupima ajali na kisha kuondoka kurudi mjini.
    “Traffic kwa Chanika adimu sana kuwaona, baada ya kutokea ajali wanaonekana tena baada ya kupiga simu ya dharura, ukifika tu Gongo la Mboto ndio utaanza kuwaona mmoja mmoja mpaka unafika Posta ndio wapo kibao, kweli kwa mtindo huu usalama barabarani ili kupunguza idadi ya vifo vinavyo sababishwa na ajali utakuwa ni hadithi kwa baadhi ya sehemu kama huku kwetu” alisema. 
    Lakini kwa upande mwingine baadhi ya wananchi hao wamempongeza kamanda wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohammed R. Mpinga kwa uchapakazi wake kwa kuzindua operesheni kadha wa kadha ikiwemo wiki ya nenda kwa usalama pamoja na kuwapa mafunzo maalum madereva wa pikipiki na kuomba askari walio chini yake wamuunge mkono kwa kufanya kazi kwa bidii na kuepuka shutuma za kuhusika na upokeaji wa Rushwa.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: