Advertisement |
Midala alisema kuanzia Januari 3 hadi januari 7 mwaka huu kulikuwepo na shida ya maji maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam hususani kwa wale wananchi wanaotumia huduma ya maji ya bomba la Ruvu chini.
Alisema bomba hilo lilikuwa limekatika,hivyo kusababisha maji mengi kumwagika,hali iliyopelekea kukosekana kwa maji maeneo mengi jijini.
Mkurugenzi huyo alisema,kutokana na kukatika kwa bomba hilo ilibidi walifanyie marekebisho ambayo yalichukuwa muda wa siku chache tokea kukatika.
"Ni kweli siku za hivi karibuni wananchi wengi walikuwa wakinilalamikia kuhusiana ukosefu wa maji lakini sasa huduma hiyo inapatikana kama kawaida kwenye maeneo yote yalikuwa yamepata usumbufu huo,"alisema Midala.
Midala alisema Sambamba na hilo DAWASCO inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya upotevu wa maji wa asilimia 50 na maji yanayopotea kibiashara.
Alisema kutokana na changamoto hizo wamejipanga kuhakikisha kuwa wezi wote wa maji wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Aidha alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano katika kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa za wizi wa maji ili kuhakikisha kila mmoja analipa bili kutokana na matumizi yake.
0 comments: