Advertisement |
KOCHA wa timu ya mpira wa miguu inayoshiriki ligi daraja la nne ya Beira FC iliyopo Chanika, Ilala jijini Dar es Salaam, Abdallah Kinyogoli 'Archeapalago' ameanzisha mashindano ya kombe la mbuzi yanayo zishirikisha timu 10.
Aliliiambia Shechambo ONLINE kuwa timu hizo zimegawanywa katika makundi mawili, ambapo kundi A limezijumuisha Chanika United inayoshiriki ligi daraja la pili, Boda boda F.C, Star Point, Mvuti pamoja na Nia njema F.C.
Pia alizitaja Nguvu Kazi FC, Beira FC, Masantula, Lukooni FC na Magari kuwa ndio timu zinazo unda kundi B.
Kinyogoli alizindua mashindano hayo siku ya alhamisi iliyopita kwenye uwanja wa shule ya Kimwani, Chanika na hadi kufikia leo zitu zote zimesha cheza mechi mbili, kundi A likiongozwa na Star Point yenye point 4 kibindoni huku Beira FC ikiongoza kundi B kwa point 4.
Aidha kocha huyo alisema dhumuni la mashindano hayo yaliyo ungwa mkono na uongozi wa timu zote shiriki, ni kuibua vipaji vya vijana kwenye soka na kuainisha kuwa kilele cha mashindano hayo kitakuwa ni Februari 2 mwaka huu ambapo mshindi atazawadiwa mbuzi mwenye thamani ya shilingi 80,000.
0 comments: