|
Advertisement |
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amemtaja mtuhumiwa aliyekamatwa na bastola Marehemu Dkt. Mvungi kuwa ni John Mayunga (56), maarufu kwa jina la Ngosha, mkazi wa Kiwalani, wilayani Temeke.
Amesema mtuhumiwa alikamatwa kutokana na ushirikiano na msaada kutoka kwa raia mwema ambaye alisaidia kutoa taarifa.
Mtuhumiwa huyo baada ya upekuzi alikutwa na bastola aina ya Revolver No. BDN 6111 pamoja na risasi 21 ambayo iligundulika kuwa ni mali ya Dk. Mvungi pamoja na baruti aina ya Explogel yenye muundo wa Sausage
Kamanda Kova, aliviambia vyombo vya habari kuwa, mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika katika tukio la kumjeruhi na kumpora Dk. Mvungi kwa kushirikiana na wenzake ambao tayari wameshakamatwa.
Kamanda Kova amesema jeshi la polisi bado wanaendelea na upelelezi ili kuendelea kuvikamata mali zingine za marehemu ikiwemo komputya mpakato (Laptop) pamoja na simu alivyokuwa akitumia marehemu na kuhakikisha kuwa vitapatikana
Alifafanua katika upelelezi wao asilimia 80 umeshafanyika.
Share This
0 comments: