|
Advertisement |
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala juzi aliwekwa kitimoto na baadhi ya wakulima wilayani Mvomero mbele ya mawaziri wengine wanne katika mkutano ulioitishwa kutafuta suluhu ya mgogoro wa wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Mkindo.
Makala ambaye pia ni Mbunge wa Mvomero ulipo mgogoro huo, alilalamikiwa na wakulima hao wakidai kwamba amekuwa akiwasikiliza zaidi wafugaji na kutoonyesha jitihada za kumaliza tatizo hilo.
Mawaziri wengine waliohudhuria mkutano huo kwa agizo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chizza, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye.
Akijibu shutuma zilizoelekezwa kwake, Makala alisema: “Msiseme tu mwangalie na juhudi zangu. Namshukuru Dk Nchimbi kwa kusoma barua ya Waziri Mkuu, uongo umejitenga na ukweli umedhihirika. Mimi nikiwa mbunge ni mwakilishi wa wananchi, nimewaita mawaziri hapa, nimekuwa kama mshenga ili wasikie malalamiko yenu,” alisema Makala
Share This
0 comments: