Thursday, November 14, 2013

Aliyoyasema Kikwete Bungeni mjini Dodoma!

ad300
Advertisement
Rais Jakaya Kikwete alizungumza na Watanzania kutoka mjini Dodoma kuhusiana na sakata zima la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Rais Kikwete alihutubia na kukabiliana na kuwapasha nchi ya Kenya, Rwanda na Uganda ambao wanaleta chokochoko za kuvunja Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC. Nchi hizo zimeibuka na kuipakazia Tanzania kuwa ndiyo inataka kuvunja umoja huo na kautaka kuitenga Tanzania jambo ambalo Rais Kikwete amelikataa. Rais Kikwete amesema Tanzania haina mpango wa kujitoa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), itaendelea kuwepo licha ya kutengwa na baadhi ya nchi wanachama. EAC inahusisha nchi tano washirika za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania ambapo kwa siku za karibuni wakuu wa nchi za Rwanda, Uganda na Kenya wanaonekana kuanzisha umoja wao ndani ya jumuiya hiyo. Rais Kikwete alisema kuwa anaamini kinachoifanya Tanzania ichukiwe na nchi nyingine wanachama wa EAC ni msimamo wa viongozi wake kuhusu ardhi, ajira, uhamiaji na uharakishwaji wa shirikisho. Alifafanua kuwa nchi ya Tanzania haijawahi kufanya lolote baya kwa nchi hizo rafiki licha ya viongozi wenzake kufanya mikutano mitatu, yaani Juni 24 hadi 25 mwaka huu, mjini Entebbe-Uganda, mkutano mwingine walifanya mjini Mombasa-Kenya Agosti 28 na Oktoba 28 walikutana tena mjini Kigali, Rwanda bila kuialika Tanzania. Amesema makubaliano ya nchi hizo tatu ni zinapofanya mambo ndani ya EAC wote wakubaliane kwa pamoja. Moja ya makubaliano aliyoyabainisha Rais Kikwete wakuu wa nchi hizo ni kuharakisha Shirikisho la EAC na kwamba itaundwa kamati ya kuandaa rasimu ya Katiba ya Shirikisho, kuharakisha uanzishwaji wa viza ya pamoja ya Utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutumia vitambulisho vya taifa kama hati ya kusafiria katika nchi zao. Ikiwemo na ujenzi wa miundombinu ya reli, barabara, usafiri wa anga na majini kuunganisha nchi za EAC ni miongoni mwa mambo ya kipaumbele cha juu yanayoshughulikiwa na jumuiya hiyo.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: