Wednesday, October 2, 2013

Kipute cha ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa (TFF) kuanza kutimua vumbi October 10 TANGA

ad300
Advertisement
Maandalizi ya mashindano ya ligi daraja la tatu ya mpira wa miguu ngazi ya mkoa Tanga yanaendelea baada ya timu kadhaa zilizomo kwenye michuano hiyo kukamilisha usajili siku ya jana baada ya kuanza shughuli hiyo majuma mawili yaliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa walimu na wasemaji kadhaa wa timu hizo, zinasema maandalizi ni mazuri hadi kufikia leo kwani mapungufu yamekuwa machache ikilinganishwa na mafanikio kwa ujumla toka kuanza kwa usajili mpaka hitimisho tayari kujiandaa na kufunguliwa kwa mashindano hayo.

Akiongea nami, Msemaji wa timu ya Lushoto Star iliyopo mjini Lushoto William Shechambo amesema timu yao imejipanga vizuri kuwakilisha wilaya yao kwenye mashindano hayo hivyo timu zote zinazotarajia kukutana nao katika mzunguko wa ligi hiyo ziwe tayari kwa mchezo wa ushindani wa hali ya juu kwani imejiandaa kushindana na kushinda si kushindwa.

"Kocha wetu Jack Franco ametumia muda na akili ya ziada kuwatengeneza vijana ipasavyo kukabiliana na michezo iliyopo mbele yetu na vijana sio siri wameiva, hivyo tunaomba tu support kutoka kwa mashabiki wote wenye mapenzi mema na timu yetu na wilaya yetu kwa ujumla" alisema Bw. Shechambo.

Naye mkufunzi wa timu hiyo Jack Franco amesema mashindano ya ligi daraja la tatu ni magumu kwani kila timu inaingia ikiwa na ari na nguvu sambamba na nia moja tu ya kupata mafanikio na kupanda daraja husika kwa mujibu wa kanuni na sheria za shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF.
 
Ligi hiyo inashirikisha timu kutoka wilaya zote za mkoa wa Tanga zilizofuzu mashindano ya mpira wa miguu ngazi ya wilaya na hivyo kupanda daraja hadi kufikia ngazi ya mkoa na inatarajiwa kuanza rasmi October 10 katika vituo vyote vilivyopo wilaya zote za mkoa wa Tanga.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: