Friday, September 27, 2013

NGASSA alipa deni

ad300
Advertisement
Kiungo anayekipiga katika timu ya Yanga ya Dar Es Salaam Mrisho Halfan Ngassa (Pichani) leo ametoa jumla ya TZS Milioni 45 kwa shirikisho la soka nchini TFF ikiwa ni sehemu ya malipo ya deni alilotakiwa kulipa ili aweze kuitumikia klabu yake hiyo aliyosajiliwa msimu wa kiangazi akitokea Simba S.C pia ya jijini Dar Es Salaam.
Ngassa amelipa deni hilo alilokuwa anadaiwa na klabu ya Simba S.C lililompelekea kukosa michezo sita za ligi kuu na kulipa faini hiyo kama adhabu aliyopewa na TFF baada ya kusaini timu mbili katika harakati za usajili.
Baada ya leo kulipa deni hilo sasa Ngassa anaruhisiwa kuanza kuichezea timu yake.
Ngassa anatarajiwa kuanza kuonekana kesho uwanja wa Taifa katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: